Wednesday, July 31

Twaendelea na Iftar ya Airtel

   ..... Tunaendelea kuwaonesha yalojiri katika Iftar iliyoandaliwa na Kampuni ya simu ya Airtel pale Serena.
    Mpangilio wa kukaa ulikua hivi...

  Kwa ukaribu zaidi, paliandaliwa very simple and classic

 Sasa ndo tukaanza yale mambo yetu yaliyotupeleka pale, hapo kuna wali wenye viungo ambao unajulikana kama wali mchafu

Halafu kuna wali mweupe ulopikwa kwa tui la nazi

  Sambusa za nyama nazo zilikuwemo, za motooooo!!

  Halafu kulikua na hivi, jina lake hatukulipata (msaada tutani Rafiqs kutujuza jina) ila ndani zilikua na mbogamboga

Chapati za kusukuma zilikuwepo, ukiziona wajua za kusukuma ila ukizila kama za maji kwa ulaini wake. Hakika msukumaji ana mkono mzuri

  Viazi ulaya vilivyokaangwa na viungo navyo vilikuwepo, juu yake vilimwagiwa vitunguu na majani yale maalumu kwa kuongeza utamu na ladha 

   Kama ilivyo ada, kwenye msosi wowote unaoandaliwa, kuku a.k.a vyuku a.k.a kwiyoooz lazima wawepo, basi hawa walitengenezwa kwa namna ya utofauti kidogo, ila mwisho wa siku utamu ulikuwepo

  Waweza jiuliza hii ilikua futari au mengineyo? Ni hivi mualiko wa futari unapotolewa, waalikwa huwa wanatoka dini tofauti wakiwemo wasio funga siku hiyo, hivyo basi inapaswa kuwafikiria wao pia na kuwatayarishia msosi ambao wataweza ula na kufurahia pamoja na wengine.
   Tutarejea kesho kuendelea na picha, maana mambo yalikua mengi atiiii!!

Tuesday, July 30

Iftar Iftar na Airtel pale Serena Ijumaa ya 26.07.2013

  Ijumaa iliyopita tulialikwa pande za Serena mjini palee.... kwenda kufuturu na Rafiqs wetu kina Airtel. Bila ajiza tulifanikiwa kufika pale na kujumuika nao. Kabla ya kuanza kujumuika tulifanya yetu yaliyotupeleka pale, ili tuweze kuwahabarisha yaliyojiri.
    Kila kitu ni mipango hata kwenye upande wa menu, lazima mipango iwekwe, na hivi ndivyo vyombo vilivyopangwa... vibakuli kwa ajili ya uji au mtori


 Kisha sahani zilikua tayari kwa matumizi

  Madishi yenye mambo yenyewe ambayo yalitukutanisha siku hiyo ya Ijumaa...

..... na vichungu vilivyobebeshwa uji pamoja na mtori ndo hivyooo

Baada ya swala ya Magharib tulijitayarisha na tende na maji kidogo

  Na kianzio ndio hiko, pamoja na chai

Kwa ukaribu...... mtori huo

  na uji wenye iliki na viungo vingine vingi ndo huoo....

    Kesho tutarejea kuwajuza zaidi kuhusiana na Iftar iliyoandaliwa na Kampuni ya simu ya Airtel pande za serena Hotel iliyopo mjini.
Share nasi Iftar uliyohudhuria nasi tutashare na Rafiqs wa Menu time hapa hapa menutimes blog.

Monday, July 29

Mtoko wa wikiendi kati ya Menu time team na Dee gatty

   Picha ilituvutia, ikatupatia hamu ya kwenda kujaribu msosi wao. Tukasema si vyema tukienda wenyewe na itapendeza zaidi tukialika marafiq wa Menu time ili waweza jaribu msosi huo nasi. 
   Kupitia mtandao wa facebook, tukawauliza Rafiqs nani angependa kuambatana nasi kwenye kuujaribu msosi wa pale Epid'or cafe, bakery & restaurant, na Dee gatty ndiye aliye penda kuambatana nasi. 
  Jumamosi muda wa chakula cha mchana ndio ahadi yetu tuliyowekeana ya kwenda pande za Epid'or cafe, bakery & restaurant.
Tulipofika baada ya kusalimiana na Anne, tulikaribishwa kinywaji hiki, chaitwa lemonade
   Kisha mwakilishi wa Menu time aliagiza hiki Surf & Turf ambayo ndani kuna "Beef steak on a bed of mashed potatoes & prawns and calamari on veggies salad on a side",

  Halafu bi Dee Gatty yeye aliagiza Sea food plate ambapo kuna "Calamari, prawns & fish fillets, with mashed potatoes, on a side there's  salad & mayonnaise sauce.

   Ndivyo ilivyoisha Jumamosi yetu pande za Masaki ilipo restaurant ya Epid'or. Tunachoweza kusema ni kwamba, chakula ni kitamu, mandhari ni nzuri, huduma ina raha na wasikizwa uzuri, halafu vyote hivi kwa gharama nafuu kabisa.
   Tujuze ya kwako iliisha vipi? tutumie kupitia menutimes@gmail.com

Friday, July 26

Kifungua kinywa cha Ijumaa

   Wikiendi si ndo hii, tunaanzaje siku??? Sisi tumeanza hivi. Chai ya maziwa kidogo, vitumbua viwili na nyama nyama kwa pembeni...


   Wewe umeanzaje? tujuze kupitia menutimes@gmail.com

Wednesday, July 24

Mchana umekaaje kwako??

  Mchana huu wa leo umepanga kupata menu gani? unaifikiria au tayari jibu unalo? Swali twakuuliza unaipata wapi? aina gani ya menu? utakua na kampani gani? utashushia na kinywaji gani?
   Sisi tunakumbushia menu tuliyopata tulipokua Sea Cliff Hotel
   Karibu kutujuza menu yako ya mchana huu, unapanga kula wapi na ni nini wataka kula.

Monday, July 22

Yaliyojiri wikiendi

   Basi kuna Rafiq zetu wameamua kushare wikiendi yao iliishaje, lakini unajua Rafiq anaposema wikiendi tuelewa siku hizi wikiendi inaanzia Jumatano hadi Jumapili.
  Ati mpaka kuna msemo, "kula bata mpaka kuku aone wivu", sasa bata huliwa kuanzia Jumatano mpaka Jumapili, hakika kuku lazma aone wivu au ashukuru kunusurika!! ila yote maisha.
  Hatuna siku kamili lini bata hili lililiwa, ila ilikua pande za Kinondoni kwa mtaalamu mwenyewe wa mambo haya, tunaongelea nyama ileee ijulikanayo kama kiti moto, a.k.a hot chair 

   Hii imechanganywa na mbogamboga, afu pembeni kuna ndizi za kukaangwa ili kukamilisha menu nzima ya wikiendi.
  Kujua ni wapi? na pia kushare nasi kuhusu yako wasiliana nasi kwa menutimes@gmail.com na +255 784 999 790
 Shukrani kwa Rafiqs kwa kushare nasi yalojiri wikiendi iliyopita.

Saturday, July 20

Mchana wa leo twala nini??

   Siku ya leo tuna swali kwako, je wala nini mchana huu? wikiendi hii?? 
  Sisi tunajirejesha nyuma siku chache tulipotembelea mitaa ya Masaki, tukasimama kwenye Hotel ya Sea Cliff na haswa restaurant ya Karambezi ambapo tulikutana na menu hii hapa.

   Moja ya menu ambayo naipenda sana ni tambi na prawns na jibini kadhaa kidhungu tunaongelea macaroni and prawns and lots of cheese.
   Ukikipenda chakula hiki, tafadhali wapitie hawa Rafiqs na jifurahishe nafsi yako. Kutoka kwetu tunawatakia kila la kheri kwenye wikiendi hii na zijazo. Stay Blessed!!

Tuesday, July 16

Chungu Cha Nne.

Matunda Matunda kabla ya uji.


Chapati za kusukuma.

Nyama, Macaron, Chapati, na Matunda

   Mwisho wa siku futar yangu ilikuwa hivi.. karibu
  Karibu tushare futari yako pamoja.

Monday, July 15

Shieni Shieni ya Sinza

   Tulikua pande za Sinza wikiendi iliyoisha,  mitaa ya Shieni bar, pale Sinza Mori, na kilichopo mezani ni chipsi iliyochanganywa na mayai a.k.a zege na ulimi ulochemshwa kisha ukamarinetiwa kabla ya kuchomwa.
    
   Pembeni pilipili kama kawa.... Rafiq, karibuni pande hizo za Sinza, ulizia walipo Shieni, huwezi jua mpishi toka Menu time anaweza kuwepo pande hizo na ukabahatika kuonja menu yake.
    Kaa chonjo! Otea uwepo wake and be there!! Tunawatakia wiki njema yenye mafanikio tele.

Friday, July 12

Nyama choma ya Kilema Moshi, Kilimanjaro

   Bado tuko pande za Kilimanjaro, Moshi, Marangu, Kilema ambako leo menu yao ya mchana ilikua ni nyama choma ya Mbuzi. Lakini kawaida yao wakikutana zaidi ya watatu tu, ni sababu tosha ya kuchinja mbuzi au ng'ombe tayari kwa starehe, huku tukishushia na mbege.
   Sasa hapo chini tayari Mbuzi keshatendewa haki

   Baada ya  muda kina baba, mangis wakawa na kazi ya kuchoma lakini kinyumbani zaidi, yaani ile ya kuwachomeka kwa vijiti afu unawasha moto na nyma inaiva taratibu.

   Ndo waishivyo Rafiqs zetu wa uchaggani, kina mangi na watoto zao. Kutoka Kilema, Moshi, asante sana Tonny kwa kutuwakilisha Menu Time.

Thursday, July 11

Machalari ya kuleee Moshi - Kilimanjaro

   Kutoka pande za Kilimanjaro, Moshi naongelea kwa wachagga, Rafiq yetu Tonny yuko pande zile na amewakilisha menu ya mchana wa leo aliyoipata, yajulikana kama ndizi nyama kimjini, ila kinyumbani ni machalari. 
   Tupate muonekano, utamu kapata yeye

  Sasa nyama imechanganywa  na utumbo, kama nawaona kina Mangi udenda unavyowatoka... Karibuni na asante sana Tonny kwa kushare nasi picha ya msosi wako.

Friday, July 5

Lunch ya Ijumaa TGIF

   Kutoka kitaani, tumekula cha mchana na bibi wa Menu Time. Eneo la mjini, mgahawa ujulikanao kwa jina la City Garden.... Karibu
   Kuna biriani ya kuku, kuna supu ya nyanya na ndizi bukoba, chapati maji na mchicha.
    Tulishushia na maji baridi na juisi ya maembe.

Thursday, July 4

Menu kutoka USA

    Kutoka kwa Rafiq, partner aliyepo pande za Obama, tunaongelea USA, aitwa Peter ameshare nasi picha ya menu aliyoipata siku ya jana.
  Karibu jionee

Tuesday, July 2

Kutoka migahawa ya Kichina

   Rafiqs, je, mwajua nini cha kuagiza pale ufikapo migahawa ya kichina?
Menu Time team tunakusaidia kukupa baadhi ya listi, na muonekano tu, ila kwenye suala la itakugharimu kiasi gani itategemea na mgahawa ulioenda.
  Cha kwanza ni sweet and sour prwans

  Cha pili ni tambi zenye mchanganyiko wa karoti na mayai

   Cha tatu ni nyama ya ngombe yenye vegetables.

    Tunaamini mko vizuri pa kuanzia, tunawatakia kila la kheri Rafiqs!!