Thursday, January 2

Mapishi ya viazi ponda vyenye vionjo a.k.a mashed potatoes

Mchana wa jana tulipata kula viazi vilivyopondwa a.k.a mashed potatoes, maharagwe pamoja na bacons
  Nataka kuwajuza namna ya kupika mashed potatoes kwa mtindo naotumia mimi, ili kupata ile ladha nayopata. Shemeji yangu aliyepata kukionja alisema "mbona kama chakula cha wagonjwa".... kwa ule ulaini na ladha yake. Karibu tupike.....

Mahitaji:
  • Viazi mviringo vilivyomenywa maganda
  • Kitunguu maji kimoja
  • Chumvi kidogo
  •  Pilipili manga kiasi
  • Blueband kiasi
  • Maziwa kiasi
  • Jibini kiasi
  • mayonnaise kiasi
Hatua:
  • Katakata viazi vilivyomenywa katika ukubwa upendao, kisha osha vizuri weka kwa sufuria tayari kwa kuchemshwa
  • Katakata kitunguu maji na weka ndani ya viazi 
  • Ongeza chumvi kiasi
  • Ongeza pilipili manga (kama wapenda)
  • Chemsha viazi vyako kwa muda wa dk 10 - 5 hadi viive kabisa
  • Baada ya viazi kuiva kabisa, chuja maji yaliyochemshia viazi kisha epua viazi vyako na weka pembeni 
  • Ongeza blue band kiasi, pamoja na maziwa kiasi, pamoja na mayonnaise bila kusahau jibini, kisha anza kuponda viazi vikiwa bado vya moto ili vionjo vyote viweze kuchanganyika kwa uharaka na urahisi. 
  • Waweza tumia kifaa maalumu cha kupondea viazi au mwiko na ponda hadi viwe vimelainika kabisa na kuondika mabongebonge yote
  • Iwapo utahisi viazi vimepondeka vya kutosha na hivina mabongebonge, basi vipo tayari kwa kupakuliwa na kuliwa.
   Muonekano utakuwa kama hivi, hapo chini:
 

  Sisi tulipata kula viazi vilivyopondwa pamoja na maharagwe pamoja na bacons ambapo kwa muonekano ilioneka hivi. Tukashushia na juisi ya mananasi pamoja na maji saf ya kunywa

  Baada ya kujaribisha pishi hili, tujuze, je ulipata ladha gani? ulifurahia? uliowapikia walisemaje nakadhalika. karibu uzungumze nasi kupitia barua pepe, tuandikie kupitia menutimes@gmail.com

No comments:

Post a Comment