So jana nikasema ngoja nijipikilishe huyo kuku asokua na mafuta, huku akisindikizwa na maharagwe pamoja na wali wa nazi wenye zabibu kavu na cooking milk.
Kumpika kuku huyu, iwapo umesahau, usipate shida nenda pale Mapishi time, kisha chagua pishi la tarehe 13, January siku ya Friday, kichwa cha habari kilikua Kuku wa kurosti na viazi, na utapata mpango mzima wa namna ya kumpika kuku huyu asohitaji mafuta wakati wa mapishi.
Tulichoongeza cha zaidi baada ya vitunguu, ni karoti moja, pilipili hoho nusu pamoja na nyanya mbili na mwisho wa pishi kuku alitokea hivi..
Kwenye upande wa wali, waupika kama kawaida ambapo tui la nazi wahakikisha halichemki, na kabla maji hayajakaukia wali wako waongeza zabibu kavu kiasi upendacho na cooking milk iwapo utapenda kuongeza ladha.
Mwisho wa upishi wali ulitokea hivi...
Maharagwe ya kopo baada ya kupashwa moto yaionekana hivi
Baada ya kupakuliwa kwenye sahani, menu nzima ilionekana hivi, na kama nilivyowaahidi kuwajuza mlo huu ulitokeaje, ahadi nimeikamilisha
Tunawatakia wikiendi njema yenye Amani na baraka, tukutane tena Jumatatu na mengi kutoka huku tulipo.
No comments:
Post a Comment