Monday, September 12

Mapishi ya Rosti ya Maini

Jioni ya leo nitashare nanyi namna ya kupika Rosti ya Maini. Waweza kula na wali, ugali, chapati, mikate au viazi au chochote unachopenda. Mie ntakuelekeza namna ya kupika rosti ya Maini halafu we utachagua utakula na nini.... Karibu!

Mahitaji:
  • Maini ya ng'ombe
  • Kitunguu swaumu kilichosagwa
  • Tangawizi iliyosagwa
  • Kitunguu maji 1
  • Chumvi
  • Mafuta ya kupikia
  • Pilipili kichaa 1
  • Biringanya 1
  • Pilipili hoho 1
  • Karoti 1
  • Viazi mviringo 2
  • Nyanya 2
  • Tui la nazi
               

           

Hatua za kupika:
  • Katakata maini katika vipande vidogo na kisha vioshe
  • Chuja maji na uweke kwenye sufuria
  • Weka sufuria kwenye jiko, washa moto na ongeza chumvi na mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi zilizosagwa
  • Acha maini yachemke, ongeza maji moto pale yanapokaukia mpaka yaive kabisa
  • Epua maini yako tayari kwa kuyaunga
  • Chukua sufuria safi, weka kwenye moto
  • Ongeza mafuta na acha yachemke kiasi kisha ongeza chumvi
  • Ongeza vitunguu maji na vipike mpaka vibadilike rangi
  • Ongeza mchanganyiko wa vitunguu swaumu na tangawizi vilivyosagwa
  • Ongeza pilipili hoho na biringanya na koroga taratibu na viache viive
  • Chukua karoti iliyokatwakatwa na viazi mviringo ambavyo utakua umevichemsha kidogo viongezee kwenye sufuria yako
  • Ongeza maini yaliyochemka, pamoja na viungo unavyopendelea
  • Ongeza nyanya na uache iivie huko ili kutengeneza rojo
  • Ongeza tui la nazi na koroga bila kuacha mpaka unapoona mboga inataka kuchemka, ila hakikisha tui halikatiki kwa kuchemka
  • Epua mboga yako tayari kwa kuliwa.
Karibuni. 

18 comments:

  1. inaonekana tam sana iyo mboga nimeipenda

    ReplyDelete
  2. jamani nilikuwa sijui jinsi ya kupika

    ReplyDelete
  3. hongera kwa pishi zuri

    EKM

    ReplyDelete
  4. Nimependa namna unavyofahamisha. Hongera

    ReplyDelete
  5. Nimependa namna unavyofahamisha, hongera.

    ReplyDelete
  6. Nimependa mapishi yako ya Rosti Maini nitapika leo jioni, Asante.

    ReplyDelete
  7. asnte sana ... unafahamisha vizuri

    ReplyDelete
  8. Dah maini haya kama umekosea hapo kutia maji na ndio mana yamepoteza muonekano

    ReplyDelete
  9. Rafiqs tunashukuru kwa maoni yenu.

    ReplyDelete
  10. Ni kweli mboga ilikua tamu sana.

    ReplyDelete
  11. Tunashukuu kupitia sisi umeweza kujua kupika, hongera kwa hilo.

    ReplyDelete
  12. EKM Asante kwa pongezi, na salamu za shukrani.

    ReplyDelete
  13. Share nasi baada ya kupika pishi hili rafiq.
    asante kwa salamu

    ReplyDelete
  14. Asante kwa salamu, ila bila ya kuweka maji nadhani yangeungua, ila waweza jaribu upishi huu bila ya kuweka maji kisha tujuze muonekano wake ulikuaje? Kwa salamu za hapo awali, sidhani kama yamepoteza muonekano ila huo ni mtazamo wako, hivyo basi tutasubiri ukipika na kushare nasi your way then tutaconfirm upi ni muonekano mwema.

    ReplyDelete
  15. asante kwa pishi hili napenda sn maini

    ReplyDelete
  16. pishi zuri, asane kwa darasa.

    ReplyDelete
  17. Mapishi mazuri ila mimi naongezea tu kwa upande wangu huwa napenda kutoa ngozi ya juu kabla sijayapika, ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete