Tuesday, October 9

Kuku choma na Ndizi

   Wanasema kupika ni popote pale unapokutana na jiko, sufuri au chombo kinginecho kinachofaa kupika pamoja na chakula cha kupika.
    Moja ya vitu navyopenda kufanya ni kupika, hivyo nikikutana na hivyo nilivyotaja hapo juu, basi hamu hunipata ghafla, halafu nikutane na Rafiqs wenye njaa basi ndo sababu inajipigia mstari vyema kabisa.
   Sehemu nyingine niliyopata kuonesha uwezo wangu wa kupika zaidi ya nyumbani kwetu ni sehemu ya makutano iliyopo kula Sinza kwa wajanja. Yaitwa Shieni bar na naamini wengi wanaijua.
    Ntakuja kukuonesha vyakula gani huwa napika pale wakati wa mwisho wa wiki a.k.a weekend, maana ndo napata muda mzuri wa kukorifisha.  Ila kwa sasa nikuoneshe moja ya menyu inayopatikana pale ambayo ni ndizi na kuku choma
 
   Ngoja nikuelekeze, ili ukitaka kupita mitaa hiyo kujaribisha mpiko wangu iwe rahisi. Kama watokea Mlimani city waelekea Mwenge, basi unakuja na njia ya pembeni kulia, unapita kanisa moja kubwa pale, halafu barabara ya kwanza mkono wa kulia unashuka nayo. Unasonga mbele, wapita matuta mawili na upande wako wa kulia utaona wachonga fanicha, kwa mbele yake kidogo ndo Shieni bar ilipo. Ni baa tulivu na yenye mandhari tulivu tu kwa kupumzika.
   Karibu upate chakula, vinywaji, utulivu huku waburudishwa na muziki laini kwa mbali.

3 comments: