Friday, December 18

Umuhimu wa Calamari a.k.a Ngisi


Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wetu, tumefanikiwa kurejea tena tukiendeleza kazi tuipendayo tulioamua kuifanya bila kushurutishwa.
  Leo tunaenda baharini na huku tunakutana na viumbe viliwavyo viitwavyo ngisi almaarufu kama Calamari an wengine humwita squid.  Kuna baadhi ya Rafiqs wanapatwa na matatizo kadha wa kadha iwapo huwala hawa viumbe, matatizo kitaalamu hujilikana kama allergies,  wengine hawapendi tu na wengine hawajui umuhimu wa viumbe hawa.
  Leo tutajuzana umuhimu wao ndani ya miili yetu, alafu kesho tutarejea kuwajuza namna mbalimbali za upishi wake ili iwe rahisi kwetu kupika  tuwapo majumbani na pia tutawajuza wanapatikana wapi kwa manunuzi yetu binafs.
 Karibuni
Hivi ni vipande vya ngisi ambavyo vimeshaoshwa na vipo tayari kwa matayarisho ya kupikwa


 Umuhimu wa ngisi ndani ya miili yetu ni pamoja na:
Kwa kuwa ina protein, basi husaidia kujenga misuli yetu. Umuhimu wa pili katika miili yetu ni zaidi kwa wale wanaofwata diet na kupenda kula kiasi na kiafya , sasa kwa menu ya ngisi kwasababu ni protein, hukaa muda tumboni vikimengenywa hivyo humpa mda mrefu wa kusikia njaa Rafiq aliyewala. 
Ngisi wana virutubisho na madini mbalimbali ikiwemo madini ya kalishium na zinc, vitamini B12, vitamini, ambavyo ni muhimu sana katika kujenga miili yetu.
   Tutarejea keshi kuwajuza zaidi wapi Ngisi hupatikana wakiwa wabichi kwa matumizi yetu mbalimbali ya nyumbani, lakini pia wale ambao wameshapikwa tayari kuliwa hupatikana wapi.
   Tufwate kupitia facebook page: Menu Time, Twitter @menutimetz pamoja na instagram @menutimes_foodtainment
    Mpaka kesho twawatakie Jumaa Kareem

Saturday, July 25

Menu ya Kitaani  Leo tupo pande za sinza kwa wajanja kwenye ile pub yetu ya mama Lulu a.k.a bibi menutime na tumekutana na foil ya ng'ombe pamoja na ndizi.
  Wameniambia hivi, pamesheni mno yaani menu za mchana kama kawa zinapatikana. Kuna bufee ambapo utakutana na menu kadha wa kadha na tutarejea kuwajuza ni menu gani.Posted by Lulu John wa Menu Time


Sunday, May 31

Yalojiri Nyama Choma Festival

     Jumamosi kumekua na matamasha kadhaa likiwemo Nyama Choma Festival, ambalo hili lilifanyika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni.
   Kama ilivyoada ni tamasha linalokutanisha wachoma nyama mahiri kutoka sehemu mbalimbali kuja kuchoma nyama ili wahudhuriaji wapate kuonja na kufurahia nyama zenye ladha tofauti tofauti 
  Baadhi ya mambo tuliyoweza kuyanasa ni pamoja na nyama zilizokua zikiendelea kuchomwa katika mabanda mbalimbali

  Moshi kutoka kwenye majiko, huku baadhi ya nyama ipo tayari kwa kuuzwa

   Wateja na wauzaji busy katika kubadilishana biashara

   Majiko ya aina tofauti katika kuhakikisha ladha kamili yapatikanika yalikuwepo

   Matayarisho zaidi, huku nyama zikiendelea kuiva jikoni

 Kwa ukaribu zaidi

  Upande wa kati ulitengwa kwa wahudhuriaji kupata sehemu ya kukaa tena chini ya kivuli wakifurahia nyama pamoja na vinywaji

   Muziki pia ulikuwepo ikiwa ni mojawapo ya viburudisho wateja walipata

    Eneo moja llikua na utofauti wa uchomaji nyama wake, yaani wao hawakutumia majiko ya kawaida kama wengine bali walichimba shimo kiasi na kuweka mkaa kisha wakazungusha vipande vya nyama vilivyochomekwa kwenye vijiti vilivyochimbiwa ndani ya ardhi kuuzunguka moto uliokua unaziivisha taratibu. Hapa Mama Menutime akipata maelezo

  Na huo ndio muonekano wa nyama zilizowekwa tayari kwa kuivishwa na makaa yanayowaka yaliyopo katikati ya mzunguko wa vipande vya nyama

  Kwa ukaribu zaidi, umahiri na ubunifu wa uchomaji wa nyama. tulipata kuambiwa kijiti chenye mguu mmoja kilikua kinauzwa shilingi elfu arubaini za kitanzania. 

  Katika kupata habari zaidi, kwenye picha hapo juu, hao ni jumla ya mbuzi kumi waliowekwa. Na kutaka kujua je utumbo na mengineyo yanakwenda wapi.... angalia picha ifuatayo

   Supu ilikua inachemka ambapo ndani yake kuna utumbo wa mbuzi wale wanaochomwa. Hivyo basi kwa mahitaji ya supu ya utumbo wa mbuzi siku hii yalipatikanika kwa hawa kina kaka wenye style ya pekee ya uchomaji wa nyama.

     Kutoka Leaders ground, ambapo NCF ilikuwepo Jumamosi ya jana, hatuna la ziada wikiendi hii. Tunawatakia wiki njema na yenye mafanikio.

Saturday, May 30

Yalojiri Goat Race event

     Siku ya Jumamosi nzuri tu ambapo shughuli ya Goat race yaani mbio za mbuzi imefanyika katika viwanja vilivyopo Masaki na kuhudhuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali Dar es salaam
    Theme ya mwaka huu ni India wear yaani mavazi ya kiasili ya wahindi. Hivyo wengi waliohudhuria walikua katika muonekano wa kiasia/ kihindi kama ilivyotakikanika na theme ya shughuli yenyewe. 
    Vyakula na vinywaji mbali mbali viliuzwa, huku michezo ya watoto ikiwepo kuwaburudisha watoto waliohudhuria.
    Tupate ushuhuda ya yalojiri katika Goat race ya 2015

Hakika walipendeza na muonekano huu

Mbuzi wakielekea kwenye uwanja wa mashindano

Kiongozi wa msafara wa mbuzi wanaoshindana

Mbuzi wamewekwa chini tayari kwa kushindana

Na mbio za mbuzi zilianza ambapo alishinda mbuzi nambari 6

Madafu, matunda yasiyo na msimu nayo yalikuwepo kupooza koo za waliohudhuria shughuli hii

Buffet kutoka Thai Kani ilikuwepo 
Pizza kutoka Bella Napoli ndio iliyoliwa na timu ya Menu Time iliyokuwepo uwanjani

 Zaidi ya hayo, kulikua na dansi za aina mbali mbali zikiwemo ngoma za kienyeji. Hatuna la ziadi kutoka viwanja vya Masaki ilipofanyika event ya Goat race 2015, 
  Tunaelekea Leaders Ground inapofanyika Nyama Choma Festival na tutarejea kuwajuza yanayojiri

Sunday, December 14

Miksi

   Pale Upanga naamini wengi twapajua maana ni mafundi wa kupika na kuuza kachori, bajia pamoja na miksi ndio waturejeshao kwenye game baada ya muda mrefu.
  Tulipita hapo na kupata miksi take away kama ionekanavyo hapo chini.
Fanya kupita hapo kuanzia mida ya saa 11 jioni.

Friday, August 29

Kilimanjaro

Ni siku nyingine tena bado twaendelea kuwajuza yalojiri pande za Moshi baada ya kurejea kutoka Arusha.
  Kama ilivyo ada tukapita pale Meku's Bistro na Rafiq aliomba  pepper steak pamoja na salad na zege
               
Na Rafiq mwingine yeye alipenda kuku makange na viepe kama ionekanavyo
Utamu wa kuijua kahawa ya Kilimanjaro ni kupitia cappuccino, hivyo nikaagiza kwa kuanzia                   
  Kisha  nikaomba pepper steak na mashed potatoes ambapo mpishi ni bwana Maulo
   
    Bado tupo hapa na tutaendelea maujuzi ya  bwana Maulo wa Meku's Bistro iliyopo Moshi.

Thursday, August 28

Mchemsho wa Arachuga

Leo tumetoka Moshi kidoogo na kwenda kutembelea pande za Arusha a.k.a Arachuga kuongea na Rafiqs mawili matatu.
   Mchana tukapata kupita Arusha park na kuagiza mchemsho kama uonekanavyo kwa picha
                           
Pia tukaagiza ugali, mchicha pamoja na mbuzi choma iliagizwa na kushushiwa na maji ya kunywa.                           
 
  Iwapo utapita pande za Arachuga fanya kama kupita pande hizi wana mengi ya kukupatia wewe Rafiq.
Twarejea zetu Moshi, endelea kuwa nasi kujua mengu ya kina Mangi

Wednesday, August 27

Moshiii

  Ilitupasa kurejea pale pa jana baada ya lile zoezi la kushare picha kwenye social media zetu na Rafiq ambaye alikua anatujoin kuomba kupata kutaste menu tulizopata jana.
   Baada ya kufika sasa menu tulizopishana nayo ni pamoja na hizi..., kuna sizzler pork na beef.
Ugali ulihusika katika kusindikizia menu hii
                                              
Na hapo sahani zote kwa pamoja                                              
Soda ndizo ziliushushia mlo wetu wa mchana.
   Kesho tunatoroka Moshi kidogo ila tutarejea jioni. Tufwate kujua Arachuga twalani

Tuesday, August 26

Moshi

  Ni Jumanne tulivu tukiwa katika mihangaiko ya kazi hapa na pale ndipo mmoja wetu akatushtua kwamba muda wa kula umewadia ila alipendekeza pia leo iwe siku ya kula nyama nyingi maana tumekuja pajulikanapo kwa upishi mzuri wa nyama.
  Mwenyeji wetu bwana Joe na Kevoo wakasema sawa tuekekee pahali pazuri kwa ajili ya ulaji wa nyama na ndipo Uhuru hostel ikateuliwa na tukafunga safari kuelekea pande hizo.
  Kufika na baada ya kutoa oda meza yetu ilitawaliwa na sahani zifuatazo hapo chini.
  Kulikua na nyama ya ng'ombe

 
 Nyama ya kondoo

 
Pamoja na nyama ya nguruwe
                                     

 Na baada ya kushiba vyema, kutokana na ukali wa jua mama Menutime alijipooza na iceceam kama ionekanavyo hapo chini.
Baada ya mlo, kama ilivyoada kupitia socia media accounts zetu tukaonesha yalojiri. Waweza tufwata kwa twitter ni @menutimetz kwa instagram ni @menutimes na facebook page ni www.facebook/menutime.com kwa habari za haraka zaidi.
  Baada ya kushare na Rafiqs mbalimbali mengi yaliibuka, kujua ni yapi tembelea blog kesho.
   Kutoka Uhuru hostel Ljm wa MT naarifu.

Monday, August 25

Twaelekea nyumbani Moshi

   Tumefika salama salimini nyumbani, naongelea Moshi, Kilimanjaro. Mkoa upendwao mno na maarufu kwa kuwa napesa maana kina Mangi wanajua kuzitafuta na kuzitumia.
  Tutakua tunajuzana mengi yatakayojiri katika safari hii toka mwanzo hadi mwisho wake tukiwa pamoja hapa bloguni au kupitia social media accounts zetu.
  Tukipofika kama ilivyo ada lazima kutia sahihi pub ya nyumbani na hivyo tulilazimika kupita Meku's Bistro kuweka sahihi kabla ya yote.
  Sahihi ya leo ilikua hiviii, samaki rosti na vikorombwezo kadhaaa akisindikizwa na viepe

   Na mwingine alisindikizwa na wali mweupe

  Ukifika round about pale huna haja ya kuuliza sana, panajionesha. Tulichopenda zaidi ni huduma nzuri hasa toka kwa bi Maria na bwana Maulo ambaye ni mpishi.
Tutarejea tena na tena na tutaendelea kuwajuza yanayojiri pande za Moshi.

Tuesday, August 5

Mwanza, Mwanza a.k.a Rock city

   Jana asubuhi tuliamkia uwanja wa ndege tukiwa safarini kuja huku kuliko na ziwa Victoria. Tunaongelea Mwanza a..k.a Rock city ambapo wale samaki watamu hupatikanika.
  Mchana wa jana tukapita Villa Park kama ilivyo ada ukifika Mwanza shurti upate kukarinishwa, na mchana walitukaribisha kwa namna hii
   Kulikua na samaki aliyekaangwa kwa mafuta tu na chumvi bila ya kiungo kingine chochote

 Visindikizio vilikua, pilipili, kachumbari, mchuzi pamoja na ugali kama vionekanavyo kwa picha hapo chini

Halafu kulikua na samaki aliyepikwa kwa viungo almaarufu kwa jina la Brenda Fasi, kama aonekanavyo hapo chini. Huyu kapikwa na viungo vingi vikiwemo karoti, pilipil hoho, ndimu, pilipili kichaa, vitunguu na kadhalika ilimradi kumnogesha na alinoga kweli kweli

   Tupo kwa muda pande za Rock city na tunaamini, tutaendeleza kuwajuza vyema yote yanayojiri pande hii. Msimu wa Serengeti Fiesta umeanza...... Ni Shiida!

Monday, August 4

Kilimanjaro, Moshi

Asubuhi tulipoamka tukajiandaa na yaliyotuleta Moshi, tukasogea meza kuu kufungua kinywa, na hivi ndio tulivyoanza siku yetu. Karibu
  Kuna kikombe cha kahawa, sausages mbili pamoja na pancakes zenye kumwagiwa syrup


   Na baada ya kufungua kinywa, tukaanza safari ya kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurejea Dar, kabla hatujaelekea Rock city, tunaongelea Mwanza.

Friday, August 1

Kilimanjaro, Moshi

  Badi tupo Kilimanjaro, Moshi na tunaendelea kuwajuza menu mbali mbali tunazozipata huku, na bado tupo Weru weru lodge tulipofikia.
  Jana jioni tulipishana na watalii wengi waliotoka na waendao kupanda mlima mrefu Afrika, tunaongelea mlima Kilimanjaro uliopo hapa hapa Moshi, Kilimanjaro, Tanzania.
  Waliotoka kuupanda walikua na kila sababu ya kusherekea kutimiza lengo lao na vinywaji vya mlipuko a.k.a champagne vilisikika kufunguliwa kila kona ya meza kusherekea utimizaji wa lengo lao la kupanda mlima mrefu Afrika, mlima Kilimanjaro.
  Wakati wanafurahia hayo, huku wengine wakiwa na shauku ya kwenda kuupanda, wana Menu Time tukajiuliza, ivi je itakuaje na sisi tukiamua kuupanda? Tujuze kama utapenda kuungana nasi iwapo hilo shauri litapendekezwa na kupita.
  Chakula cha usiku tulipata hapahapa Weru weru lodge na udhibitisho ni huu hapa chini. Kama kawaida tulianza na supu
Ilikua ni supu ya mboga mboga, na pembeni tulichukua kipande cha mkate pamoja na salad, ili kulainisha tumbo kabla ya mlo kamili.

  Kisha tukaingia kwenye mlo kamili kama ionekanavyo hapo chini
  Mtindo wa usiku ilikua ni buffeet ambapo kulikua na aina mbalimbali za vyakula na kwenye sahani yetu tulichukua kabichi zilizokaangwa, kipande cha kuku aliyekaangwa na viungo, beef lasagne, kabab za samaki, viazi vilivyookwa pamoja na ugali uliopikwa kimexco yaani una maziwa na cheese.
   Tulishushia na glasi ya mvinyo mwekundu na kushukuru siku imemalizika vyema.
 Tutarejea kuwajuza zaidi kuhusu menu nyingine tutakazozipata bado tukiwa hapa.
  Kutoka Kilimanjaro, Ljm naarifu!!

Thursday, July 31

Kilimanjaro, Moshi

   Asubuhi ya leo tumedamka na kuelekea nyumbani yaani Kilimanjaro, Moshi, na tutaishia Moshi mjini pasi kufika Rombo mkuu kwa bibi.
   Hoteli tuliyoshukia ni Weru weru Lodge ambayo ina mandhari nzuri mno, na utulivu wa hali ya juu.
  Mchana ulipotimu tuliagiza mlo kwa ajili ya kupoza njaa, na kujitoa na uchovu wa safari.

Rafiqs karibuni kushuhudia menu yetu ya mchana kutoka hapa
  Tulianza na supu yenye vipande vya kuku na uyoga, na kwa ushahidi pata picha hapo chiniKwa mlo kamili tulipata kuagiza chipsi pamoja na nyama ya steak, vikisindikizwa na salad kidogo na sauce pembeni kwa ajili ya kuilia hiyo nyama
   

 Kutokana na hali ya ubaridi, tulipendelea kupata Cappuccino katika kusindikizia mlo huo, na hiki ni kikombe ambacho tulitayarishiwa
      

 Tutaendelea kuwajuza menu kadha wa kadha tutakazopata hapo, kadri ya siku tutakazoishi hapa.
Kwa kupata habari kwa uharaka zaidi tufwate instagram kupitia @menutimes pia twitter tunafwate kupitia @menutimetz na kwenye face book page yetu ni www.facebook/Menu time.com

Friday, July 11

Tuanze wikiendi nyingine pamoja

  Wikiendi si ndo inaanza, leo sisemi sana nakujuza kuwa iwapo utataka kupata menu hiyo hapo ambayo ni samaki walipikwa na viepe ndani ya foili, basi ifwate Shikamoo pesa bar iliyopo Sinza kwa wajanja.
  Zaidi ya menu hiyo, kuna biriani, kokoto, mbuzi katoliki toka kwa jirani, mihogo ya kukaanga na chachandu yake na mengineyo mengi huku ukishushia na vinywaji mbalimbali bariiiidi na muziki murua. 
 Kaka Fredy anasema, Karibuni

Thursday, July 10

Wikiendi ndefu na menu zake

  bado twaendelea kukujuza yalojiri katika hii long wikiendi ambapo ilianza Ijumaa hadi Jumatatu ambapo tulikua tunatimilisha sikukuu ya wakulima hapa tanzania.
  sasa siku ya Jumapili, tulipata kwenda kuosha macho viwanja vya sabasaba nikiwa na mama yangu, na baada yakutoka hapo na kufaidi mengi, tukaona tupite mgahawa mmoja katikati ya mji ujulikanao kama Mokka City lounge na menu tuliyoipata ni hii hapa chini...... karibuni
  Mimi kama kawaida yangu nilipata menu hii ambapo ipo hivi, ni vimikate vya pizza ambavyo ndani kuna vipande vya nyama ya kuku na viungo vingine, huku ikisindikizwa na salad pamoja na mayonnaise

Mama yeye alipata kujaribisha biriani ya kuku, na moja ya neno alitoa ni kwamba biriani hii ilikosa lile rojo la kibiriani ambalo walipata kitaani au mtu akilipika home, Uzuri mwisho wa siku alipata kuenjoy jinsi ilivyo maana upishi watofautiana, na ilikua ni vyema kujaribu mapishi mengine.

   Fanya kuwapitia hawa Mokka City lounge waliopo mjini katikati iwapo mida ya menu itakupata eneo hilo, au iwapo wataka kujaribisha mapishi ya aina tofauti.
   kutoka kwetu, kutoka wikiendi ndefu ndo tunakomea hapa na tutarejea kesho tuanze kuangalia wikiendi hii twaanzia wapi. Karibu kutujuza wapi mtakuwepo wewe na marafiki zako kupitia anwani yetu menutimes@gmail.com