Tuesday, August 28

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa Kisukari - Siku ya Kwanza

  Kama tulivyoahidi, tutaanza kuzungumzia ni chakula gani Rafiqs wa magonjwa mbalimbali wanaposwa kula ili kuimarisha na kuijenga vyema miili yao.
   Tumeanza na Rafiqs wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Na tutazungumza chakula kipi anapaswa ale katika wiki nzima kwa mujibu wa waganga a.k.a doctors, na leo tutaanza na Siku ya kwanza. Karibuni sana....
   Tafadhali elewa kwamba Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni.

  KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya, Mkate vipande viwili (mweupe au wa brown)
 
 SAA 4 ASUBUHI
  •  Juisi freshi au kikombe cha chai au tunda

 CHAKULA CHA MCHANA
  • Ndizi mchemsho ,Samaki mchemsho na mbogamboga

 SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda 

 CHAKULA CHA USIKU
  • Viazi mviringo mchemsho na mbogamboga na tunda

    Tumemaliza mlo wa siku ya kwanza kwa Rafiqs wanausumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Naamini vimeeleweka vyema na vinaweza kupikika na kutayarishika.
    Karibu kuuliza maswali, kutupatia maoni na lolote lingine kama unalo kupitia anwani zetu ambazo ni menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com.
    Tunamshukuru Mganga a.k.a Doctor kutoka Lugalo hospital iliyo Dar iliyo salama kwa kutupatia ufahamu huu ambao tunashare nanyi.

5 comments:

  1. Asanteni kwa hii diet jaman..it is really very helpful. but as a request. mnaweza pia kutueleza jinsi ya kutengeneza/kupika vyakula mnavyotuonyesha?

    ReplyDelete
  2. Asante kwa swali, tafadhali angalia upande wa vipengele kwenye Mapishi time, huko tunaonesha namna tofauti za mapishi .

    ReplyDelete
  3. ahsante kwa kutuelimisha lakini ni matunda gani mgonjwa wa sukari anaweza kutumia? viazi vitamu pia anaweza kutumia?

    ReplyDelete
  4. AHSANTE KWA KUTUELIMISHA NAMNA YA KUTUMIA VYAKULA.NI MATUNDA GANI MGONJWA WA KISUKARI ANAWEZA KULA? VIAZI VITAMU VIKITUMIWA NA MGONJWA WA SUKARI HAKUNA TATIZO?

    ReplyDelete
  5. Mgonjwa wa kisukari anaruhusiwa afanye mapenzi mara ngapi kwa wiki?

    ReplyDelete