Wednesday, September 28

Upishi wa vitumbua

Nilipokua Mwanza, katika pitapita zangu za hapa na pale, asubuhi moja nkakutana na mama mmoja ambae anapika vitumbua. Vilikua vitamu na laini wala sikuhitaji shushia na chai, juisi sijui maji, yaani vyenyewe viliteremka.
Sababu tayari nilimkuta ameshaandaa kila kitu na kilichobaki ni kuvikaanga tu, basi nikaomba anihabarishe jinsi alivyoviandaa. Akanijuza vyema nami nashare nawe, Alisema: Kutokana na wingi wa vitumbua mmoja anaamua kupika basi ujazo hutofautiana
  • Unachukua mchele, kisha unauosha na kuuanika juani, ukishakauka unausaga
  • Unachukua unga wa mchele unachanganya na wa sembe na wa ngano
  • Unaukoroga pamoja huku ukiupika mpaka uive kabisa
  • Unauacha upoe, kisha unaweka hamira chapa maandashi na ya chengachenga(kijiko kimoja cha chai) ili uumuke vyema. Unauacha uumuke kwa masaa 4 hadi 5
  • Unaongezea yai moja kisha unakoroga vyema, unaongeza na sukari kiasi unakoroga vichanganyike vyema
  • Baada ya hapo unaweka kikaangio motoni, unaweka mafuta kidogo kwenye kila tundu na kumimina ule mchanganyiko wako
  • Kwa kutumia vifimbo vya mishkaki unageuza pale upande wa chini unapoanza kugeuka rangi na kuwa brauni na kukiondosha kinapokua kimeiva
  • Kitumbua chako kitakua tayari kwa kuliwa

Kama una namna ingine ya upishi wa vitumbua tafadhali tutumie kupitia menutimes@gmail.com nasi tutawajuza wengine

2 comments:

  1. Asante nashukuru. Ni njia ndefu kidogo lakini kitu kizuri kina gharimiwa. Ila vipimo hukuweka k.m. unga wa mchele kiasi gani, wa ngani/mahindi kiasi ganina maji kiasi gani. Je nikiamua kuloweka mchele na kuusaga kwenye blender kabla ya kuuanika vitatokea? Asante

    ReplyDelete
  2. Asante kwa maoni. Ni kweli hatukuweka vipimo kwani mama huyu mpishi tulipishana naye katika biashara na alitueleza kwa uchache. Tutafanyia kazi maoni yako na kutafuta vipimo sahihi na maelekezo yaliyojitosheleza na kuwaletea. Asante na endelea kututembelea.

    ReplyDelete