Wiki iliyokwisha niliahidi kueleza mahitaji na hatua za upishi wa pilau, na pia nilisema nitaonesha kwa picha hatua kwa hatua ili sote tujifunze mapishi ya pilau.
Karibuni tujifunze kupika pilau.
Mahitaji:
· Mchele kilo 2
· Nyama ya mfupa kilo 2
· Vitunguu maji 2 na karoti kubwa 2
· Viungo vya pilau vilivyosagwa pakiti moja(saizi ya kati)
· Viungo vya pilau visivyosagwa
· Chumvi kiasi
· Mafuta ya olive
· Njegere glasi
· Viazi ulaya nusu kilo
· Vitunguu swaum
Hatua:
Chemsha nyama yako mpaka iive, uwe umeweka chumvi kiasi, hakikisha nyama ina supu ya kutosha wakati wa kuichemsha
Osha mchele wako tayari kwa kuutumia na kisha utenge pembeni
Weka sufuria jikoni, kisha ongeza mafuta. Yakisha pata moto weka vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kuaanga viive. Ongeza chumvi kiasi na endelea kukoroga
Ongeza vitunguu swaumu vilivyopondwa na endelea kukoroga, koroga mpaka vitunguu vigeuke kuwa rangi ya kahawia na kuiva
- Ongeza viazi ulaya, vilivyomenywa na kukatwakatwa kwa ukubwa uupendao, endelea kukoroga ili vipate kuiva
Ongeza njegere na endelea kukoroga ili vipate kuiva
Ongeza vipande vya nyama iliyochemka vyema ndani ya mchanganyiko wako. Koroga mchanganyiko huo na acha kwa dakika chache uive vyema
Na hivi ndo itakavoonekana baada ya dakika kama 10 hivi ulizoacha mchanganyiko uive vyema
Supu uliyochemshia nyama itakua inaonekana hivi baada ya kuondoa nyama. Yaonekana tamu kunyweka ila usiinywe inahusika sana kwenye pishi letu
Sasa ndo tunaanza kuweka viungo vya pilau na tunaanza na vile ambavyo havijatwangwa. Anza na iliki huku unaongeza maji pale yanapokauka
Ongeza viungo vingine naongelea abdalasini, weka pakiti zima (saizi ya kati), weka binzari nyembamba pia na koroga ili vichanganyike vyema. Lazma harufu nzuri utaisikia maana mchanganyiko wa viungo hivi una harufu tamu mnoo
Ongeza ile supu tuliyoiweka kando ndani ya mchanganyiko huo
Sasa ongeza viungo vilivyosagwa ndani ya supu na mchanganyiko wako
Acha mchanganyiko uweze kuchanganyiko vyema huku vikichemka kwa dakika kadhaa na hivi ndo itakavoonekana
Sasa chukua ule mchele wako ulioukosha na weka ndani ya sufuria yako , koroga kidogo kisha acha uweze kuiva
Baada ya dakika kama 5 angalia chakula chako, kumbuka kupunguza moto pale maji yanapoanza kukauka. Angalia wali kama umeanza kuiva na kama bado haujaiva na maji yamepungua basi ongeza maji huku unaacha viweze kuiva vyema
Hivi ndio itakavyoonekana pale pilau yako itakapoanza kuiva vyema. endelea kupunguza moto kwani tayari menyu inakaribia kuiva
Raha ya kula pilau na ili inoge vyema kachumbari lazima iwepo. Kuna namna nyingi ya kuzitengeneza ila mie binafsi napenda yenye vitunguu maji, nyanya, ndimu na chumvi baasi. Na hivi ndio kachumbari yangu ilionekana
Pakua pilau yako tayari kwa kuliwa na wageni, familia, rafiq zako. Sisi ya kwetu ilionekana hivi baada ya kupakua
Namshukuru wifi yangu Caroline kwa kunifundisha na kuniruhusu kupata muongozo wote huu mpaka kufanikisha pishi hili la pilau. Iwapo utajaribu tujuze lilitokeaje kupitia menutimes@gmail.com
ahsante sana kwa kutufahamisha vipi kupika pilau, picha zake zinafanya ujifundishe hapo hapo na ule...
ReplyDeleteNimependa maelekezo yako yanayoambatana na pichq ,hakika twajifunza vyema.
ReplyDeleteDuuu tamuu sana
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKiukweli ilikua tamu sana. Ijaribu nawe kisha tujuze ilikuaje??
ReplyDeleteAsanteni kwa maoni yenu, tutahakikisha tunaendelea kuwafundisha huku tukitumia picha nyingi tuwezavyo.
ReplyDeleteAsante mpendwa kwa kutujuza mapishi ya pilau.Binafisi nimefurahi saana. Thanks!
ReplyDeleteWoow tamujeee, i will have to try thz one weekend
Deletenjegere unaweka zikiwa mbichi ama unachemsha kidogo kwanza,
ReplyDeleteAHSANTE NDUGU KWA MAFUNZOYAKOYAUPISHIWA PILAU.
ReplyDeleteJEE KAMASINA NJEGERE NAWEZA KUTUMIA NIN IBADALA YAKEE.