Sunday, March 4

Mapishi ya Pilau- kama tulivyoahidi

   Wiki iliyokwisha niliahidi kueleza mahitaji na hatua za upishi wa pilau, na pia nilisema nitaonesha kwa picha hatua kwa hatua ili sote tujifunze mapishi ya pilau.
Karibuni tujifunze kupika pilau.

Mahitaji:
·         Mchele kilo 2
·         Nyama ya mfupa kilo 2
·         Vitunguu maji 2 na karoti kubwa 2
·         Viungo vya pilau vilivyosagwa pakiti moja(saizi ya kati)
·         Viungo vya pilau visivyosagwa
·         Chumvi kiasi
·         Mafuta ya olive
·         Njegere glasi
·         Viazi ulaya nusu kilo
·         Vitunguu swaum  

Hatua:
  • Chemsha nyama yako mpaka iive, uwe umeweka chumvi kiasi, hakikisha nyama ina supu ya kutosha wakati wa kuichemsha
  • Osha mchele wako tayari kwa kuutumia na kisha utenge pembeni
  • Weka sufuria jikoni, kisha ongeza mafuta. Yakisha pata moto weka vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kuaanga viive. Ongeza chumvi kiasi na endelea kukoroga
  • Ongeza vitunguu swaumu vilivyopondwa na endelea kukoroga, koroga mpaka vitunguu vigeuke kuwa rangi ya kahawia na kuiva
  • Ongeza viazi ulaya, vilivyomenywa na kukatwakatwa kwa ukubwa uupendao, endelea kukoroga ili vipate kuiva



  • Ongeza njegere na endelea kukoroga ili vipate kuiva



  • Ongeza vipande vya nyama iliyochemka vyema ndani ya mchanganyiko wako. Koroga mchanganyiko huo na acha kwa dakika chache uive vyema



  • Na hivi ndo itakavoonekana baada ya dakika kama 10 hivi ulizoacha mchanganyiko uive vyema 



  • Supu uliyochemshia nyama itakua inaonekana hivi baada ya kuondoa nyama. Yaonekana tamu kunyweka ila usiinywe inahusika sana kwenye pishi letu 



  • Sasa ndo tunaanza kuweka viungo vya pilau na tunaanza na vile ambavyo havijatwangwa. Anza na iliki huku unaongeza maji pale yanapokauka



  • Ongeza viungo vingine naongelea abdalasini, weka pakiti zima (saizi ya kati), weka binzari nyembamba pia na koroga ili vichanganyike vyema. Lazma harufu nzuri utaisikia maana mchanganyiko wa viungo hivi una harufu tamu mnoo 



  • Ongeza ile supu tuliyoiweka kando ndani ya mchanganyiko huo 



  • Sasa ongeza viungo vilivyosagwa ndani ya supu na mchanganyiko wako  



  • Acha mchanganyiko uweze kuchanganyiko vyema huku vikichemka kwa dakika kadhaa na hivi ndo itakavoonekana



  • Sasa chukua ule mchele wako ulioukosha na weka ndani ya sufuria yako , koroga kidogo kisha acha uweze kuiva 



  • Baada ya dakika kama 5 angalia chakula chako, kumbuka kupunguza moto pale maji yanapoanza kukauka. Angalia wali kama umeanza kuiva na kama bado haujaiva na maji yamepungua basi ongeza maji huku unaacha viweze kuiva vyema



  • Hivi ndio itakavyoonekana pale pilau yako itakapoanza kuiva vyema. endelea kupunguza moto kwani tayari menyu inakaribia kuiva



  • Raha ya kula pilau na ili inoge vyema kachumbari lazima iwepo. Kuna namna nyingi ya kuzitengeneza ila mie binafsi napenda yenye vitunguu maji, nyanya, ndimu na chumvi baasi.  Na hivi ndio kachumbari yangu ilionekana



  • Pakua pilau yako tayari kwa kuliwa na wageni, familia, rafiq zako. Sisi ya kwetu ilionekana hivi baada ya kupakua 



  • Namshukuru wifi yangu Caroline kwa kunifundisha na kuniruhusu kupata muongozo wote huu mpaka kufanikisha pishi hili la pilau. Iwapo utajaribu tujuze lilitokeaje kupitia menutimes@gmail.com

    10 comments:

    1. ahsante sana kwa kutufahamisha vipi kupika pilau, picha zake zinafanya ujifundishe hapo hapo na ule...

      ReplyDelete
    2. Nimependa maelekezo yako yanayoambatana na pichq ,hakika twajifunza vyema.

      ReplyDelete
    3. This comment has been removed by the author.

      ReplyDelete
    4. Kiukweli ilikua tamu sana. Ijaribu nawe kisha tujuze ilikuaje??

      ReplyDelete
    5. Asanteni kwa maoni yenu, tutahakikisha tunaendelea kuwafundisha huku tukitumia picha nyingi tuwezavyo.

      ReplyDelete
    6. Asante mpendwa kwa kutujuza mapishi ya pilau.Binafisi nimefurahi saana. Thanks!


      ReplyDelete
      Replies
      1. Woow tamujeee, i will have to try thz one weekend

        Delete
    7. njegere unaweka zikiwa mbichi ama unachemsha kidogo kwanza,

      ReplyDelete
    8. AHSANTE NDUGU KWA MAFUNZOYAKOYAUPISHIWA PILAU.
      JEE KAMASINA NJEGERE NAWEZA KUTUMIA NIN IBADALA YAKEE.

      ReplyDelete