Thursday, March 1

Unapajua KT Shop

   Mjini Dar Es Salaam, huku Tanzania kuna duka linalojulikana sana kwa bajia, sambusa, kabab na zagazaga kibao. na vionjo kama chetna, chachandu na pilipili pale ndo nyumbani kwao.
   Kuna chai ya iliki, masala n,k yaani ubao wao wa yaliyomo ni mrefu mno. Duka hili lipo mda mrefu mno, zaidi ya miaka 30 iliyopita. Laitwa KT shop na kingine nachopenda toka duka hili ni huduma unapewa fasta na hawaringi hawa, wapo kibiashara zaidi.
   Nakuonesha menyu nayopenda zaidi kila napokwenda KT shop

Kababs:

Bajia:


 Chetna yenye machicha ya nazi

KT shop ipo mkabala na Chef''s pride. Pita hapo upate utam asee

No comments:

Post a Comment