Sunday, September 11

Mapishi ya Mtori

Namna ya kupika Mtori... Hapa nafundishwa na mama yangu mzazi, na kasema huu ni mtori ambao alikua anapika kwao Rombo, Moshi.
Mahitaji:
  • Nyama ya ng'ombe
  • Ndizi mbichi
  • Kitunguu maji
  • Mafuta ya kupikia
  • Blue band / Tanbond
  • Chumvi kiasi
Namna ya Kupika
  • Katakata nyama na kisha iweke kwenye sufuria yenye maji kidogo na chumvi kiasi
  • Chemsha nyama mpaka iive
  • Epua nyama yako na uiweke pembeni
  • Menya maganda ya ndizi
  • Katakata ndizi katika vipande vidogo kisha vioshe
  • Weka ndizi kwenye sufuria lenye maji kiasi na chumvi
  • Katakata vitunguu maji na viongeze kwenye sufuria lenye ndizi
  • Chemsha ndizi
  • Mara kwa mara geuza ndizi na mwiko ili kuhakikisha zote zinaiva.
  • Epua ndizi zako, na kisha punguza maji uliyochemshia kwenye chombo safi
  • Pondaponda ndizi huku ukiongeza maji uliyoyatenga ili kulainisha mchanganyiko
  • Ongeza Blueband/ Tanbond huku ukiendelea kuponda
  • Ndizi zinapokua laini kabisa weka nyama uliyochemsha kwenye mchanganyiko wa ndizi
  • Ongeza maji uliyochemshia nyama na koroga mpaka mchanganyiko huo uchanganyike vyema
  • Mtori wako upo tayari kwa kuliwa
Karibu........

1 comment: