Friday, September 9

Mwanza Mwanza ...

Naendelea kukuletea picha za baadhi ya maeneo ya Mwanza a.k.a Rock City. Tunasafiri pamojah au sio.... tusafishe macho pamojah.

  • Humu ndio nilipokua naishi katika siku huzi chache. niliambiwa hii meli ilikua inafanya kazi kipindi cha nyuma, na baadae imegeuzwa kuwa sehemu ya Hotel Tilapia, kuna vyumba kama 6.

  • Kutoka barazani kwangu ghorofa ya kwanza, niliweza pata picha na mandhari nzuri. Siku moja jioni nilikutana na mandhari hii, Kamera ikapata mshawasha wa kutumika... Ilikua mida ya jioni kuelekea usiku:
  • Na nyakati za mchana mandhari hiyo hiyo huonekana  huonekana hivi
  • Hapa bwana ndio utambulisho wa sasa kwamba umepita Mwanza, shurti upige picha na huyu samaki. basi unakuta kuna wapiga picha wapo hapa kwa biashara hii kila siku asubuhi. Usiku mashine inazimwa na samaki anaacha kutoa maji. Kwa wasanii sehemu muhimu hii, na kwa maharusi nimehabarishwa tukitoka kanisani lazma tupite hapa kukamilisha album. Karibu Mwanza


Kutoka Mwanza a.k.a Rock city ni hayo tu..... tukutane nkirejea Dar es salaam, ila kama unataka kutujuza kuhusu chochote toka mkoa wowote karibu sana, tutumie kupitia menutimes@gmail.com.

No comments:

Post a Comment