Friday, September 9

Menyu ya kihindi ndani ya Mwanza

Raha ya kusafiri ni kuona sehemu mbalimbali na kusafisha macho, mie nikaendeleza mpaka kusafisha na mdomo kabisaaa kwa kujaribu ladha tofauti tofauti.
Sijawahi kuongelea menyu toka kwa wenzetu wa India, ila ni mpenzi wa chakula chao, na mara kwa mara wakati natoa oda huwa nawaomba wasiweke kiwango cha pilipili kama cha kwao, maana waweza shindwa kula ukawa unauguza ulimi kupooza ile pilipili.
Mwanza nilikutana na mapishi ya Chicken curry na Romali roti, hizi ni chapati flain wameniambia zinapikwa kwenye mkaa. Ntatafuta khabari yake zaidi kisha niwajuze, ila ni tamu na hazina mafuta sana.

No comments:

Post a Comment