Mwaka jana tulipata bahati ya kualikwa kwa Dada Mage a.k.a Megvicta. Huyu mwanadada ndie aliyetufunza ile menyu ya kuku wa kukaanga kiaina.
Moja ya mapishi alipika ni matoke, lakini picha ilichukuliwa na kaka Lucian na ametuletea tuweze kushare nanyi. Sasa kinachofuatia ni kuwasiliana na Da Mage atufunze na kutujuza hili pishi la matoke, ila kwa leo tufurahie picha.
Rafiq, kama wajua namna ya kupika matoke waweza kutujuza kupitia menutimes@gmail.com wakati tunasuburia toka kwa Da Mage.
MT inawashukuru Da Mage na Kaka Lucian kwa kushirikiana nasi
Wow, will get to you na maelezo yote ya jinsi yakuandaa matoke.yummmmmmm
ReplyDeleteAsante sana Da Mage. Tunasubiri kwa hamu namna ya kujifunza hili pishi. MT
ReplyDeleteJinsi ya kupika matoke:
ReplyDeleteTayarisha ndizi mbichi aina ya Bukoba, nyama, maharage meupe au ya soya, nyanya chungu, nyanya, nyama, kitunguu maji, roiko.
Menya ndizi na kuziosha kwenye maji safi.
Weka ndizi kwenye sufuria kubwa yenye nafasi ya kutosha,weka nyama bila supu, weka maharage yalichemshwa kidogo, weka nyanya vitunguu na nyanya chungu ongeza ndizi nyingine juu, tia maji yafunike ndizi kidogo, funika na jani la mgomba kwa radha zaidi au sinia.
Chemsha mpaka maji yaishie, ongeza chumvi kidogo, roiko na supu ya nyama chemsha mpaka ndizi na maji vimeshikana. Ndizi zako zitakuwa tayari pakua. NB: Sijaweka mafuta kwa afya ile supu ya nyama inatosha.
,
Asante kwa kutujuza
ReplyDeleteAsante,nazipenda sana hizo ndizi,namna ya kuzipika
ReplyDeleteilikua shida.