Thursday, January 19

Menyu ya asubuhi

    Kila mmoja wetu ana namna ya kufungua kinywa, hii sote tunakubaliana nayo. Kwa wanaoenda makazini au biasharani siku za Juma (na wengine hadi jumamosi) ni ngumu kwa kiasi flani kupata ile menyu ya asubuhi tunavyoitaka wenyewe. Yaani kutokana na kukimbizana na kuwahi basi unajikuta unafungulia kinywa katika maeneo ya shughuli zako zinapofanyika.
   Kwa siku ya Jumapili kama imekaa kifamilia zaidi, pale waweza kunywa chai unatumia masaa 2 na zaidi, unaongea na familia kidogo, unasoma magazeti au majarida taratiiibu huku unafaidi kikombe cha chai au kahawa au chochote unachokunywa.
   Naamini ndo maana hata wengi tunapenda kukutana kwa chakula cha asubuhi changanya na cha mchana a.k.a brunch siku za Jumapili.
   Kutoka HongKong, rafiq ametutumia kifungua kinywa alikua anapata. Na alipopatia paitwa Zentro bar n grill. Siku ukitembelea huko usisite kupita, na kama upo huko fanya hivyo basi kisha utujuze.

  Tunaelekea mwisho wa wiki, naamini wengi tutapata muda wa kufungua vinywa na familia zetu. Piga picha menyu mtakayojipatia asubuhi ya wikiendi hii kisha tutumie.
  Au tufanye kashindano kadogo hivi, tuletee picha kupitia menutimes@gmail.com halafu wasomaji wa Menutime blog ndio watakua majaji. Zawadi itatolewa na familia ya MenuTime, na mpaka Jumatatu tutasema ni zawadi ni nini.

1 comment:

  1. mmmh,basi naingia hilo shindano! zawadi ni nini?

    ReplyDelete