Friday, January 20

Karibu sokoni a.k.a Shopping

   Sote tunakula walau mara moja kwa siku, wengine mara mbili, na kama tunavyoshauriwa mara tatu kwa siku yaani mlo wa asubuhi, mchana na jioni.
   Wapi tunapata mahitaji yetu? tunatofautiana kutokana na sababu mbalimbali, iwe umbali, ukaribu, uwezo wa kifedha, aina ya mahitaji, uchaguzi wa mahitaji n.k
    Kuna masoko, naongelea kariakoo, kisutu, kulikua na mahakama ya ndizi karibu na mabibo pale, kuna soko la ilala, kuna la mbezi n.k na naamini katika maeneo kadhaa lazima kutakua na soko ili kukimu mahitaji ya wakazi wa pale.
   Ukiondoa masoko kuna magenge, haya yapo sehemu kadhaa pia, na uzuri wa haya magenge ukitoka kwako sekunde kadhaa unapata mahitaji yako, labda mwenye genge ale mtaji au awe mzembe wa kutokuhakikisha stock anayo ya kutosha.
  Halafu kuna maduka makubwa a.k.a Supermarkets , haya yapo sehemu chache na kuna mini markets ambazo zipo kwa wingi. humu unapata zagazaga kibao upande wa mapishi hadi vinavyotumika kupikia naongelea sufuria, vikaangio, mwiko n.k, pia utapata sahani na wenzie.
  Katika pita pita zetu Tyikson alikutana na genge mitaa flani hapa Dar iliyo Salama.

  Magenge mengi tunanunua mahitaji yetu kwa mafungu na sio kwa kilo, japokuwa kuna yanayouza kwa kilo, kama atakua na mizani. Kuna mpaka ubuyu, chumvi yenye ndimu yaani chaguo ni lako.
  Wewe unapata mahitaji yako wapi? tujuze kupitia menutimes@gmail.com ili tupatembelee tuweze kuwajuza wengine.


Kutoka gengeni, TYI wa MT naarifu

3 comments:

  1. Mpendwa kikubwa tunachosubiri ni recipe jitahidi ukitoa menu na recipe iwe karibu kuna matoke umetoa picha watu mate yametudondoka recipe hamna hadi leo but gud job tunakukubali

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa January 20. 4:45 PM tunashukuru kwa ushauri wako tutalizingatia hilo usiwe na shaka karibu sana. Menu Time Team

    ReplyDelete
  3. Naamini uliipata ile recipe ya matoke. Angalia kwenye post ya matoke kwenye comments na utaiona. Kuna baadhi ya picha tunatumiwa bila recipe na inachukua muda kidogo mpaka Rafiq aturejee na recipe yake. Tuvumilie tukichelewa.

    ReplyDelete