Monday, January 16

Ubunifu

  Katika pitapita zetu tulikutana na menu book ambayo ipo tofauti kidogo, binafsi nilivutiwa. Nahisi waliwafikiria watu wa aina tofautitofauti wanaokuja hii sehemu yao na walijaribu kubuni namna ya kuonesha yaliyomo katika mgahawa wao na bei wanayotoza.
  Uhalisia wa picha mara nyingi unavutia flani, yaani inakua rahisi mtu kujua mlo huu unafananaje haswa kwa zile menyu ambazo hatujaizoea saaana. Ofcourse kila mtu anajua chipsi zikoje au wali ukoje ila kuna menyu nyingine kuanzia kwenye jina linaloandikwa hadi kwenye muonekano zinapokuja mezani, zinakuacha hoi, huchelewi kuomba maelekezo namna ya kula.
  Sasa hawa ndugu zangu wapo KIA (Kilimanjaro International Airport) kama nakumbuka vyema katika mgahawa mmoja hivi. Ukifika unaangalia menu inakupa picha na bei hapo hapo, sasa utata utabaki kwenye kubadilisha pesa za kigeni kwenda za madafu kimahesabu lakini, ila wanakusaidia fasta.

  Karibu kuona ubunifu wao, hii ni moja ya kurasa inayoonesha vyakula:
Na hii inaonesha vinywaji:


Imependeza, Inavutia, Inarahisisha yaani hutumii nguvu sana kwenye kutoa oda.

No comments:

Post a Comment