Monday, July 2

Safari Lager Nyama Choma Festival June 30.

Ilikuwa ni Safari Lager Nyama choma Festival ya 2012,T-Bonaz, hawa watu Jovin na George asee walitisha sana, waliichoma nyama na nyama ililika yoooote... na bado tulikuwa tunahitaji zaidi na zaidi..
Banda hili lilikuwa na kuku na wooooote waliisha... hivi unapata picha watu wanavopenda nyama, hawa wote waliliwa... duh.
Kuku akichomwa kwenye wavu wa chini baadae uhamishiwa wavu wa juu ili waive sawa sawa.
Ng'ombe na mbuzi choma katika hatua za awali za kuchomwa.

Shawarma ilikuwepo na ilikuwa katika banda pekee unajipatia Shawarma yako basi burudaani tupu.





Mchomaji wa hii kitu alinambia inaitwa Bomu ina mchanganyiko wa maini, Kuku, ng'ombe na mbuzi afu inachomwa katikka fuko moja.
Hapa bomu kama limeiva hivi....
Hivi ndivo ilivokuwa pale katika viwanja vya Posta Kijitonyama, Jumamosi ya Tarehe 30 June 2012. We are Menu Time, Karibu.

1 comment: