Wednesday, February 29

Mayai ya kukoroga a.k.a Scramble eggs

   Leo tuone namna ya kutengeneza mayai ya kukoroga au kuvuruga kama wengi wanavyopenda kuyaita, lakini kwa lugha ya wenzetu yaitwa scramble eggs.
   Moja ya vyakula ambavyo huwa navionesha kwenye facebook na kuulizwa namna ya kupika mara nyingi ni mlo huu.
  Sasa karibuni tupike mayai....
Mahitaji:
·         Mayai mawili
·         Pilipili hoho nusu
·         Nyanya nusu
·         Kitunguu maji nusu
·         Chumvi kiasi
·         Mafuta ya olive kiasi
·         Maziwa robo kikombe
·         Tomato paste
·         Jibini

Hatua:
Katakata viungo vyote na weka kwenye vyombo tofauti, Koroga mayai yako tayari kwa kupika
Weka kikaango jikoni baada  ya kuwasha jiko, ongeza mafuta vijiko viwili, weka chumvi kiasi, kisha ongezea na vipande vya vitunguu maji, koroga mpaka viive na kuwa rangi ya kahawia.  

Ongeza pilipili hoho na koroga mchanganyiko wako. Kisha weka nyanya na endelea kukoroga mpaka nyanya iive na kutengeneza kama rojo flani. Weka mayai huku unayakoroga koroga, na kabla hayajakauka ongeza maziwa na endelea kukoroga 

Ongeza tomato paste kidogo, koroga, na malizia kuweka cheese (waweza tumia jibini ngumu kisha kaikwaruza au unanunua iliyo ya maji tayari) Koroga mchanganyiko huo mpaka uive vyema.Pakua mayai tayari kwa kuliwa 

Chemsha maziwa uliyoyakoroga na milo na sukari kidogo (kama utapenda kuongeza sukari) na yakishachemka weka kwenye kikombe tayari kwa kunywa  

Na hivi ndo mlo utaonekana, maana wa kwangu ulionekana hivi. 

Waweza kula na kinywaji kingine zaidi ya maziwa ni wewe tu na mapenzi yako. karibu ujaribu kupika mayai ya kuvuruga.  

No comments:

Post a Comment