Tuesday, February 28

Pita ........ Ukutane navyo, Uvione, Uvionje

   Katika pitapita za hapa na pale za wanaMenuTime, moja ya menyu walikutana nazo ni hizi hapa:

   Hii ni meza wamewekwa vipande vya kuku, ambapo vinauzwa kwa bei tofauti kufuatia ukubwa wake. Wanaanzaia shilingi 1,000 - 2,500 ya kitanzania. Wengi hununua na kuvila hivyo hivyo au kuvipika kama mboga na kula na mlo mwingine kama ugali, wali, viazi n.k.
   Meza hii ilikutwa Mbagala, Dar es salaam, Tanzania.

    Toka Mbagala hadi Kigamboni ambapo ilikutwa mbuzi foil, ugali, maharagwe na mchicha wa kusindikizia menyu nzima. Natamani sana kujua pishi hili la foil, ila kutokana na kukutwa tayari ishapikwa basi ikabidi timu ile na kupata picha tu, ila ni kiporo tutakachofanyia kazi.
   Share nasi unachokutana nacho mitaani kupitia menutimes@gmail.com

No comments:

Post a Comment