Kama ilivyoada ni tamasha linalokutanisha wachoma nyama mahiri kutoka sehemu mbalimbali kuja kuchoma nyama ili wahudhuriaji wapate kuonja na kufurahia nyama zenye ladha tofauti tofauti
Moshi kutoka kwenye majiko, huku baadhi ya nyama ipo tayari kwa kuuzwa
Wateja na wauzaji busy katika kubadilishana biashara
Kwa ukaribu zaidi
Eneo moja llikua na utofauti wa uchomaji nyama wake, yaani wao hawakutumia majiko ya kawaida kama wengine bali walichimba shimo kiasi na kuweka mkaa kisha wakazungusha vipande vya nyama vilivyochomekwa kwenye vijiti vilivyochimbiwa ndani ya ardhi kuuzunguka moto uliokua unaziivisha taratibu. Hapa Mama Menutime akipata maelezo
Na huo ndio muonekano wa nyama zilizowekwa tayari kwa kuivishwa na makaa yanayowaka yaliyopo katikati ya mzunguko wa vipande vya nyama
Kwa ukaribu zaidi, umahiri na ubunifu wa uchomaji wa nyama. tulipata kuambiwa kijiti chenye mguu mmoja kilikua kinauzwa shilingi elfu arubaini za kitanzania.
Katika kupata habari zaidi, kwenye picha hapo juu, hao ni jumla ya mbuzi kumi waliowekwa. Na kutaka kujua je utumbo na mengineyo yanakwenda wapi.... angalia picha ifuatayo
Supu ilikua inachemka ambapo ndani yake kuna utumbo wa mbuzi wale wanaochomwa. Hivyo basi kwa mahitaji ya supu ya utumbo wa mbuzi siku hii yalipatikanika kwa hawa kina kaka wenye style ya pekee ya uchomaji wa nyama.
Kutoka Leaders ground, ambapo NCF ilikuwepo Jumamosi ya jana, hatuna la ziada wikiendi hii. Tunawatakia wiki njema na yenye mafanikio.
No comments:
Post a Comment