Siku ya Jumamosi nzuri tu ambapo shughuli ya Goat race yaani mbio za mbuzi imefanyika katika viwanja vilivyopo Masaki na kuhudhuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali Dar es salaam
Theme ya mwaka huu ni India wear yaani mavazi ya kiasili ya wahindi. Hivyo wengi waliohudhuria walikua katika muonekano wa kiasia/ kihindi kama ilivyotakikanika na theme ya shughuli yenyewe.
Vyakula na vinywaji mbali mbali viliuzwa, huku michezo ya watoto ikiwepo kuwaburudisha watoto waliohudhuria.
Tupate ushuhuda ya yalojiri katika Goat race ya 2015
Hakika walipendeza na muonekano huu
Mbuzi wakielekea kwenye uwanja wa mashindano
Kiongozi wa msafara wa mbuzi wanaoshindana
Mbuzi wamewekwa chini tayari kwa kushindana
Na mbio za mbuzi zilianza ambapo alishinda mbuzi nambari 6
Madafu, matunda yasiyo na msimu nayo yalikuwepo kupooza koo za waliohudhuria shughuli hii
Buffet kutoka Thai Kani ilikuwepo
Pizza kutoka Bella Napoli ndio iliyoliwa na timu ya Menu Time iliyokuwepo uwanjani
Zaidi ya hayo, kulikua na dansi za aina mbali mbali zikiwemo ngoma za kienyeji. Hatuna la ziadi kutoka viwanja vya Masaki ilipofanyika event ya Goat race 2015,
Tunaelekea Leaders Ground inapofanyika Nyama Choma Festival na tutarejea kuwajuza yanayojiri
No comments:
Post a Comment