Sunday, May 22

Mapishi ya keki

Leo tutaangalia namna ya kupika keki ya Chokoleti.
Kuna urahisi kwenye namna ya kupika endapo utanunua unga ambao tayari umechanganywa na michanganyiko kadhaa tayari kwa kupika keki, na unachohitaji kufanya ni kuongeza baadhi ya viungo kidogo kisha kuiweka kwenye jiko la Oven tayari kwa kuoka.

Mahitaji:
 • Unga uliyotayarishwa tayari kwa kupikwa (pakiti moja - 500g)
 • Mayai matatu
 • Mafuta ya kupikia 80ml
 • Maji safi 200ml
 • Butter kiasi
Kwa ajili ya topping
 • Nunua chokolate yenye karanga
 • Maziwa kikombe kimoja • Hatua za kupika:

 • Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 sentigrade (365F)
 • Paka butter kiasi kwenye kikaangio chako kisha kiweke pembeni
 • Koroga mayai, changanya na maji safi, mafuta ya kupikia pamoja na unga uliyotayarishwa mpaka vichanganyike vyema
 • Nyunyuzia unga wa cocoa au unga wa ngano katika kikaangio chako ulichokipaka butter
 • Weka mchanganyiko wa unga, mayai, mafuta ya kupikia pamoja na maji safi ndani ya kikaangio chako
 • Ingiza ndani ya oven na funga mlango uache keki iive kwa dakika zitegemeazo aina ya kikaangio chako.
 • (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya mstatili na kina vipimo hivi: 5 X 33 X 22cms = 2 X 13 X 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 - 45 kupika keki yako).
 • (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 22cms = 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 - 45 kupika keki yako).
 • (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 15cms = 6 inches basi utatumia muda wa dk 55 - 60 kupika keki yako).
 • Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita
 • Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko
 • Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga
 • Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 - 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio
Namna ya kutengeneza topping:
 • Weka sufuria safi kwenye jiko
 • Vunja vunja chokolate yako na iweke kwenye sufuria yenye moto
 • Ongeza maziwa kikombe kimoja yenye moto
 • Koroga mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vyema
 • Epua mchanganyiko wako weka na anza kupaka kwa kutumia brashi kwenye keki yako ambayo itakua imeshapoa
 • Keki yako ipo tayari kwa kuliwa
Waweza kula na soda, chai, juice, maji, maziwa au hata peke yake. 
                      
       
Karibuni !!

6 comments:

 1. we hujui kupika!!! unanunua peketi iliyochanganywa tayari, mshamba we

  ReplyDelete
 2. Asante sana kwa maoni yako.
  Naomba uangalie post ya Jumatatu tarehe 25, mwezi wa July 2011, utaona namna ya kupika keki toka hatua za awali. Namaanisha kuanzia kuchanganya unga mpaka keki kuwa tayari.
  Sio kila mmoja wetu ana muda wa kuchanganya unga na mahitaji mengine toka mwanzo. Na upishi huu wa kutumia unga uliotayarishwa na kuongezea viungo vichache ni maalumu kwa wale wasio kua na muda au wasiopenda kusimama jikoni muda mrefu.
  Asante tena kwa kutembelea blog hii.

  LJM.

  ReplyDelete
 3. Jamani keki hii haina sukari? Mmmhhh

  ReplyDelete
 4. Asante kwa salamu Dadaz4life.
  Baadhi ya mahitaji yaliyotumika kutengenezea yana mathani unga uliyotayarisha kabisa una sukari ya kutosha

  ReplyDelete
 5. Mmmmh, nimependa hii, kazi simple sana!

  ReplyDelete