Friday, August 31

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa Kisukari - Siku ya Pili

   Tunaendelea na ratiba yetu, chakula gani kiliwe au kitayarishwa kwa Rafiqs wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.
 Narejea ushauri kuwa, Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni

KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya au chai ya maziwa na Soya, Mkate vipande viwili (mweupe au wa brown)
 
SAA 4 ASUBUHI
  •  Juisi freshi au maziwa au tunda
 
CHAKULA CHA MCHANA
  • Ugali wa dona, kuku mchemsho na mboga mboga
 
SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda 

CHAKULA CHA USIKU
  • Viazi mviringo mchemsho na mbogamboga na kachumbari ya karoti (mbichi)
 
   Mlo wa siku ya pili ndo umeishia hapo, kwa Rafiqs wanausumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Naamini vimeeleweka vyema na vinaweza kupikika na kutayarishika.
    Endelea kuuliza maswali, kutupatia maoni na lolote lingine kama unalo kupitia anwani zetu ambazo ni menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com.
    Tunaendelea kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mganga a.k.a Doctor kutoka Lugalo hospital iliyo Dar iliyo salama kwa kutupatia ufahamu huu ambao tunashare nanyi.

No comments:

Post a Comment