Saturday, September 1

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa kisukari - Siku ya Tatu

   Tunazidi kusonga mbele kuelimishana kuhusiana na chakula gani kitayarishwa kwa Rafiqs wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari., siku ya tatu leo!!
Kumbuka tena kuwa, Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni
     Karibuni:

KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya au chai ya maziwa na Soya,Ndizi za kuchemsha

SAA 4 ASUBUHI
  • Juisi freshi au tunda

CHAKULA CHA MCHANA
  • Ugali wa ulezi, Samaki mchemsho, mboga mboga na tunda

SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda

CHAKULA CHA USIKU
  • Wali, mbogamboga na tunda

   Siku ya tatu itakua imekwisha vyema baada ya mlo huo hapo juu ulioelezewa vyema. Tuna imani kuwa vimeeleweka vyema na vinaweza kupikika na kutayarishika.
   Endelea kutupatia maoni, kutujuza, kuuliza maswali au lolote lingine kama unalo kupitia anwani zetu ambazo ni menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com.
    Shukrani zetu bado zinabaki Dar iliyo salama, pale hospitali za Lugalo kwa kutupatia ufahamu huu ambao tunashare nanyi

No comments:

Post a Comment