Saturday, August 25

Matibabu ya Mnin'ginio!!!

   Tupo kwenye Wikiendi na Wikiendi zina mambo mengi sana. Kikawaida kwa wale tusiofanya kazi Jumamosi siku ya Ijumaa ndo mwanzo wa Wikiendi, japokua siku hizi kuna msemo ati "Thursday is new Friday", kwa mantiki hiyo basi wenye msemo huu wanaanza Wikiendi siku ya Alhamisi, sio????
   Menu Time ipo kwa ajili yenu katika kuhakikisha katika njia moja au nyingine inawaletea habari zenye manufaa kwa wote. Leo tuongelee nini kifuate baada ya shughuli za mwisho wa wiki a.k.a Weekend. Kama nlivyosema mengi hutokea, maana kumbi za starehe ndo siku ya kuingiza faida, na kwenye hilo lazima makampuni yanayohusika na uuzaji wa vimiminika iwe vyenye au visivyo na ulevi, makampuni yote ndo muda wa kuuza
  Sasa basi, tukishamaliza kutoa ushirikiano wetu na makampuni haya, haswaaa yanayohusiana na vimiminika vyenye kilevi, iwapo tunapitiliza ushirikiano wetu,,,,,,, basi siku inayofuatwa ndipo mning'inio a.k.a Hang over inatusumbua sana baadhi yetu!! Menu Time imeliona hili, ikasema ni vyema kulifanyia kazi.
   Ukiwa pande za Kigoma, na umeamka na mnin'ginio, usihofu, jivute Kizota bar paleeee, kisha pata mambo kama hayo hapo chini

  
Ni supu ya kuku wa kienyeji, iliyochemshwa na viazi tu bila ya kikorombwezo chochote, na pembeni sasa kutokana na mapenzi yako wamekuwekea vikorombwezo hivyo, kina pilipili, limau na chumvi.
   Ukipata hiyo, tena ya moto, ukajitahidi na walau chapati mbili, ukashushia na maji baridi, kwa wengine watashtua na moja baridi, basi siku yako itaenda vyema.
   Asanteni Kigoma mwisho wa reli, nimefurahi kupata ujuzi wenu.
Rafiq wa Menu Time tujuze je, una njia gani ingine ungependa Rafiqs wa MenuTime waitumie baada ya kuifahamu kupitia Menu Time blog katika kukata mning,inio.
   Kutoka Kigoma, Menu time wanaarifu!!!

2 comments:

  1. We need more details on Mning'inio

    ReplyDelete
  2. Tutafanyia kazi ombi lako, tusamehe kwa kuchelewa kukurejea

    ReplyDelete