Friday, August 24

Kifungua kinywa a.k.a Breakfast toka Zanzibar

    Kutoka visiwa vinavyonukia karafuu, vyenye mashamba ya viungo vya kila aina, tuongelee kuanzia vya chai, pilau, mboga na kadhalika, visiwa vyenye historia za utumwa na mengi ya kale pia, naongelea visiwa vya Zanzibar, tunapata kujua wanafungua vinywa kivipi.
   Rafiq wa menu Time alikua pande za huko katika shughuli za kuendesha taifa na moja ya kifungua kinywa alichopata ni hicho picha yake hapo chini.
   Kuna mkate uliookwa, bacons, mayai ya kuvuruga a.k.a scramble eggs pamoja na sausages. Vyote alivisindikiza na chai maziwa yenye kahawa na sukari kwa mbali.

   Menu Time inawajali sana, tena sana katika maswala ya msosi, na afya zetu. Na kwa kusema hivyo na kudhibitisha, tutakuja kuwajuza ni menyu ipi Rafiq awe anapata akiwa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali.
   Tutakua tunapata msaada wa habari za ukweli na uhakika toka kwa madaktari na dietician, yaani wale wataalamu wa mambo ya milo, kutoka hospitali za Lugalo hapa Dar iliyo salama, tutawajuza mengi na tunaamini yatatusaidia sana.
   Kwa kuanzia tutaongelea ni menyu gani, Rafiq anayesumbuliwa na ugonjwa wa kisukari a.k.a diabetes anapaswa au anashauriwa kula ili kuweza kuishi salama zaidi. Tukutane wiki ijayo tukianza mada hiyo.
  Kutoka Zanzibar, shukrani sana kwa Ephraim Junior. Menu Time tunawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki!!

No comments:

Post a Comment