Friday, December 18
Umuhimu wa Calamari a.k.a Ngisi
Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wetu, tumefanikiwa kurejea tena tukiendeleza kazi tuipendayo tulioamua kuifanya bila kushurutishwa.
Leo tunaenda baharini na huku tunakutana na viumbe viliwavyo viitwavyo ngisi almaarufu kama Calamari an wengine humwita squid. Kuna baadhi ya Rafiqs wanapatwa na matatizo kadha wa kadha iwapo huwala hawa viumbe, matatizo kitaalamu hujilikana kama allergies, wengine hawapendi tu na wengine hawajui umuhimu wa viumbe hawa.
Leo tutajuzana umuhimu wao ndani ya miili yetu, alafu kesho tutarejea kuwajuza namna mbalimbali za upishi wake ili iwe rahisi kwetu kupika tuwapo majumbani na pia tutawajuza wanapatikana wapi kwa manunuzi yetu binafs.
Karibuni
Hivi ni vipande vya ngisi ambavyo vimeshaoshwa na vipo tayari kwa matayarisho ya kupikwa
Umuhimu wa ngisi ndani ya miili yetu ni pamoja na:
Kwa kuwa ina protein, basi husaidia kujenga misuli yetu. Umuhimu wa pili katika miili yetu ni zaidi kwa wale wanaofwata diet na kupenda kula kiasi na kiafya , sasa kwa menu ya ngisi kwasababu ni protein, hukaa muda tumboni vikimengenywa hivyo humpa mda mrefu wa kusikia njaa Rafiq aliyewala.
Ngisi wana virutubisho na madini mbalimbali ikiwemo madini ya kalishium na zinc, vitamini B12, vitamini, ambavyo ni muhimu sana katika kujenga miili yetu.
Tutarejea keshi kuwajuza zaidi wapi Ngisi hupatikana wakiwa wabichi kwa matumizi yetu mbalimbali ya nyumbani, lakini pia wale ambao wameshapikwa tayari kuliwa hupatikana wapi.
Tufwate kupitia facebook page: Menu Time, Twitter @menutimetz pamoja na instagram @menutimes_foodtainment
Mpaka kesho twawatakie Jumaa Kareem
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment