Friday, October 5

Maini ya kuku rosti

   Moja ya chakula, ambacho ni rahisi kupika na ni kitamu na pia nakipenda ni maini ya kuku. Iwe yamekaangwa, yamechomwa, yamerostiwa yaani wakisema tu kuwa kuna maini ya kuku, mie huyoooo nshafika. Mara nyingi maini huandaliwa na firigisi ila kwa sababu ambazo bado sijazijua, wakinipatia vyote basi firigisi zitaliwa na Rafiq mwingine.
   Hapa nakuonesha moja ya msosi uliohusisha maini ya kuku. Ni Ugali mweupe pamoja na maini ya kuku yaliyorostiwa vikisindikizwa na mbogamboga.
 
  Hii menyu inapatikana sehemu nyingi, ila mara nyingi mie naifuata kwa wajanja Sinza, iliyopo Dare es salaam. Pale kuna baa yaitwa Shieni.
   Leo nitakuwepo pale, ambapo nitapika maini pamoja na firigisi na marafiq watakaokuwepo watakula, kisha ntaja kuwajuza yaliyojiri. Pia nitawaeleza nimeyapikaje ili nawe ujaribu kisha uturejee.
   Hii ni ijumaa na ndo mwisho wa wiki. Menu Time inawatakia Ijumaa na Weekend njema

No comments:

Post a Comment