Wednesday, October 3

Menyu ya Kitaani

   Mchana ikitukutia barabarani, yaani kitaani kwenye mizunguko afu tukaamua tupate chakula cha mchana, mara nyingi itakua sehemu wanapika nyama iwe wa mbuzi, ng'ombe, kitimoto n.k, maana lazima mboga hiyo tutaishushia na ugali na mboga mboga za majani.
   Wiki iliyopita katika pitapita za mtaani, pande za Ilala, pale miami bar, tulikutana na ugali wao, nyama ilikua ni ya mbuzi na pembeni mbogamboga za kusindikizia.

    Ugali waja na kachumbari, na mchicha ulokaangwa na vitunguu maji
 
   Kisha waletewa mbogamboga nyingine ambayo ni mchanganyiko wa nyanya chungu na bamia, zilizoungwa vyema tu kuleta virutubisho mbali na utamu uliomo.
 
   Na mwisho, laja sinia lenye nyama ya mbuzi iliyochomwa kwa utaratibu na utaalamu wa hali ya juu, ni laini na tamu kiukweli. Upande tuliochagua ulikua ni mbavu, na tukaletewa kama inavoonesha pichani hapo chini
   
   Share nasi ukiwa kitaani ni mlo gani unapenda kula, au wajikuta unaula mara kwa mara kutokana na mazingira yaliyokuzunguka. Email address zetu ndo zile zile. Karibu!!

No comments:

Post a Comment