Tuesday, October 2

Yaliyojiri katika Safari Nyama Choma Festival - Jumamosi iliyopita

   Safari Nyama Choma Festival ilikuwepo Jumamosi iliyopita pale viwanja vya Posta kule maeneo ya Sayansi. Menu Time team tulikuwepo tukiwasindikiza T.bonaz team.
    Nakujuza yaliyojiri kwa picha ili tuende sawa.

Hapo T.bonaz team wameweka T.bones tayari jikoni
 
Kwa mbali kidogo muonekano ndo uko hivi, na hii ni kwa upande wa juu wa moja ya jiko kati ya matatu yaliyokua yameandaliwa.

Hapa sasa mambo yanaanza kuiva vyema...... oda kibao zinangoja nyama iive
 
Kisindikizio kilikua ndizi, za kuchoma ambazo hata kwenye picha inaonesha jinsi gani zachomwa kwa mbaliiiii na moto wa mkaa, na zinaiva ivoo!! 
 
 
Menu Time salads zilikuwepo, kuna ile ya mayonnaise afu na ile ya kibongo yajulikana kama Menu Time Bongo salad
 
Kwenye bakuli yaonekana hivi. Ilitumika kusindikiza wala nyama iliyonunuliwa toka kwa T.bonaz. ka pilipili kenye ujuzi toka India nako kalikuwepo pande za hapo ili kuhakikisha ladha inayopatikana hapo ni tamu muno!
 
Kutoka viwanja vya Postal ground kwenye tamasha hilo la Safari Nyama Choma Festival, Menu Time team we are signing out!!

No comments:

Post a Comment