Monday, January 6

Upishi wa Vibawa vya kuku a.k.a chicken wings & chipsi

   Usiku wa leo tumeona tupike chakula rahisi tu, kwa kutengeneza pamoja na kukila. Hivyo basi tunapika chipsi zilizomaliziwa kwa kutandaziwa jibini kwa juu, kachumbari yenye mayonnaise pamoja na vibawa vya kuku vilivyokaangwa kisha kumaliziwa na samli, pilipili pamoja na gin.
  Tunaamini sote twajua kukaanga chipsi, ila kukupa utamu wa mapishi ya menu time, fanya hivi:

  • Ukishakatakata viazi vyako, osha vizuri kisha weka kwenye sufuria, katika kitunguu maji na chumvi kidogo kisha chemsha kwa dakika chache ili viazi vipate kulainika vyema
  • Epua na chuja maji yote kisha kaanga kwenye mafuta ya moto 
  • Kwaruza jibini na tandaza juu ya chipsi zilizotoka kuepuliwa mara. 

Muonekano wetu ulikua hivi

    Vibawa vya kuku tulivipika kwa mtindo huu:

  • Tuliviosha vyema, kisha tukaweka chumvi, vinegar na ndimu kidogo kwenye bakuli pembeni, tukakoroga vyema kisha kumwagia vibawa na kuviacha vikipata mchanganyiko huo kama nusu saa
  • Tukaweka kikaangio chenye mafuta jikoni, kisha tukakaanga vibawa huku tukivigeuza baada ya kuiva upande mmoja
  • Baada ya kuhakikisha wameia pande zote, tuliepua vibawa vya kuku
  • Tukaweka kikaangio kingine motoni, tukaweka samli a.k.a butter, pamoja na pilipili ya maji (waweza tumia ya kukatakata iwapo wapendelea) kisha tukakaanga na kuongeza gin (sio lazima) 
  • Tukaviweka vipande vya mabawa ndani ya kikaangio na kuvikaanga kwa muda ili kuhakikisha vinachanganyika vyema na mchanganyiko wa kwenye kikaango
  • Tukaepua baada ya kuhakikisha mchuzi wote umeisha kwenye kikaango kwa kunyonywa na vibawa, na vibawa vya kuku vipo tayari kwa kuliwa
Muonekano wetu ulikua hivi

   Kwenye salad, vilitumika vifuatavyo: nyanya, kitunguu maji, tango, mayonnaise pamoja na chumvi kidogo. Unaviosha vyema kisha katakata katika ukubwa wa kiasi, na kuvichanganya pamoja na mayonnaise, na muonekano ulikua kama hivi

  Na hicho ndicho chakula chetu cha usiku wa leo, ni rahisi kupika na rahisi kukila.

   Tunakutakia jioni njema, na muendelezo wa wiki njema. Tupo kwenye twitter @menutimetz, instagram @menutimes,  facebook page yetu ni www.facebook.com/MenuTime.  na barua pepe ni menutimes@gmail.com. Karibu tuwasiliane

No comments:

Post a Comment