Tuesday, January 7

Menu ya wanafamilia walipopata mtoko wa pamoja - pande za Seacliff

   Familia yangu inathamini kile nachofanya, hivyo mara kwa mara huwa wanashare nami, menu tofautitofauti wanazopata pale wanapokumbuka kupiga picha. 
 Tukubali ukweli kupiga picha chakula inahitaji uwe na upendo wa pekee na chakula na mara nyingine watu waliokaa pembeni yangu hushangaa kwanini napiga picha chakula kabla ya kula.... mara nyngine nawajibu nipo kazini.
   Kutoka Dar iliyo salama kula Masaki, seacliff, ndugu zangu walipata kutoka kwa chakula cha usiku na ushuhuda wao ni huu hapa
 Kuna pork ribs na viepe

 Kuna viepe na prawns a.k.a kamba

 Nachopenda zaidi macaroni yenye kamba a.k.a prawns
  
 Mishkaki ya samaki, salad, wali na sauce kwa pembeni

   Asanteni sana wanafamilia kwa kunikumbuka na kunipatia cha kupost siku ya leo. Nafarijika na nashukuru Mungu kuwa mmoja wa wanafamilia yangu. Mwenyezi Mungu atuzidishie zaidi 2014.
   Kutoka Sea cliff, wanafamilia wa Lulu John M wametujuza!!

No comments:

Post a Comment