Wednesday, January 1

Kheri ya Mwaka Mpya 2014!!!!

   Hongereni sana sana kwa kufika mwaka mpya, mwaka mwingine 2014, ambapo tunaomba Baraka, Amani, Upendo,Ushirikiano, Umoja viendelee kuwepo ndani yetu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
   Tunaamini tuna kila sababu ya kufurahia kufikia hapa na kuwaombea wale wote wenye shida, matatizo, magonjwa na kadhalika kupata wepesi katika vyote wanavyokumbana nayo
  Uongozi mzima wa Menu time unapenda kuwashukuru wote kwa mchango wenu, changamoto mnazotupa, maoni, maswali, ushari mbalimbali katika kuhakikisha tunawapatia kile mnapenda.
Tunaahidi kujiboresha zaidi na pia kuendelea kuwanufaisha wengine kupitia njia nyiginezo zikiwemo magazeti na kadhalika mbali na mitandao ya jamii kama blogu, twitter, facebook na instagram
  Tunaomba muendelee kujumuika nasi, kutushauri, kutukosoa, kutuongoza na kusoma habari zetu mwaka huu 2014 pamoja na mingine ijayo
   Tunawapenda sana na tunawatakia kila a kheri kwenu na familia zenu!!

    Mwenyezi Mungu atubariki sote !!!

No comments:

Post a Comment