Tuesday, June 26

Vitafunwa.

Binadamu ni wabunifu sana pale linapokuja swala la menu, wameweza kubuni sambusa za aina mbalimbali, hapa tunazo sambusa za nyama na huweza kuliwa wakati wowote, lakini mara nyingi watu huzipendelea asubuhi kama kitafunwa.
 Chapati pia ni zao la ubunifu wa binadamu katika harakati za kuandaa Menu.
 Mkate ni miongoni mwa vyakula vya kwanza kabisa kugundulika, na inasadikika kuwa ni miongoni mwa vyakula vilivodumu karne nyingi kuliko vyakula vingine.
 

Monday, June 25

Wali Mweupe.

Wali mweupe a.k.a majimaji waweza kuliwa na mboga za aina mbali mbali, hii itategemea na upatikanaji wa mboga, mahala ulipo au mapenzi yako wewe mlaji. MT imeonelea ni vema tukaona mboga zinazopendelewa na wakazi wengi wa Tanzania.

Wali nyama, ni moja ya menu inayopendwa na wakazi wengi wa Tanzania na inapatikana kwa urahisi pia.
 Wali wa samaki pia unapatikana na unapendwa sana, ukiingia hoteli yoyote Tanzania, wali samaki ni moja kati ya menu kuu.
 Ningeisahau wali kuku wadau wangenitoa macho, wali kwa kuku ni moja kati ya menu nzuri na tamu sana, awe kuku wa kukaanga ama wa mchuzi.
 Karibu Tanzania, Karibu Wali Mweupe lakini piaaaaa Karibu Menu Time.

Sunday, June 24

Mnuso wa Uncle Ringo (Exclusive)

Katika harusi mbalimbali na sherehe mbalimbali, hakuna sehemu muhimu na inayopendwa na watu wengi kama muda wa msosi a.k.a Menu Time, Uncle Ringo na Aunt Anitha Jumamosi ya tarehe 23 June 2012, walizikonga nyoyo zao kwa kufunga pingu za maisha, zilizofuatiwa na sherehe kubwa na ya kistaarabu iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, MT ilishuhudia mwanzo mwisho idara ya maakuli na hii hapa ni exclusive coverage ya Mnuso wa Uncle Ringo.


 Ndafu ni moja kati ya menu nyingi zilizokuwepo, Mshereheshaji wa siku hiyo alitoa historia ya kitu hii kuitwa ndafu na kusema kuwa, hii ilitokea baada ya Mzungu mmoja kukaribishwa Menu Hii huko Moshi, Baada ya kuiona tu na kuionja mzungu wacha maneno yamtoke, akasema "This is Wonderful" wakazi wa Moshi waliokuwepo eneo hilo wakasema Mzungu kaiita "Ndafu", Kuanzia siku hiyo mpaka leo Hii kitu inaitwa Ndafu.
Hatukuishia kwenye ndafu tu, tulienda hatua nyingi mbele zaidi tukakutana na kitu cha  Buffet, wali mweupe a.k.a majimaji ilikuwa nambari wani.
Bila wali mchafu a.k.a Pilau sidhani kama viwanja vya Karimjee vingekalika ha ha ha ha sherehe bila pilau haijatimia.
Wale wenzangu na mimi wa ndizi hawakusalimika kwenye Buffet la Mnuso wa Uncle Ringo, Acha watu wajilie kitu cha ndizi.
Kabla sijaelewa nini kinaendelea mbele yangu nikakutana na vipande vingi vingi vya kuku, acha niduwaee, ama kweli macho yatashindwa kutambua vitu vingine lakini sio chakula.

Ng'ombe nao hawakusalimika, ilibidi wachinjwe na wapikwe Rost, ali mradi Kusherehesha Harusi ya Mr& Mrs. Ringo.
Wataalamu wa chakula wanayaita Macaron, matamu hayo.
Ki ukweli aina nyingi za vyakula zilikuwepo na ulikuwa huru kuchagua mlo uupendao, Samaki walokatwa vipande vipande, wakakaangwa, kisha wakaandaliwa na mchuzi, niliionja na ilikuwa tamu mno.
Mboga mboga na Kisamvu pia vilijumuishwa kwenye Mnuso.

Salad iliandaliwa ya kutosha na mtu alikuwa huru kula salad aipendayo, chagua ya kwako na wewe kati ya hizi.



Dah! mimi niliridhika na maandalizi ya sherehe nzima na lilipokuja swala la Menu niliwakubali sana waandaaji. tupe mtazamo wako na wewe. Kama una sherehe yako na ungependa Menu Time tuiripoti wasiliana nasi.

Friday, June 22

The Safari Lager Nyama Choma Festival, Dar es salaam.

Dar es salaam tena, Ni Safari Lager Nyama Choma Festival Pale pale kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama. kwa kiingilio cha sh. 5000 tu kwa watu wazima na 3000 kwa Wanachuo. Kuanzia saa sita mchana mpaka saa tano usiku tarehe 30,June 2012 (Jumamosi).
 Kama ilivo ada Timu Ya Menu Time Tutakuwepo na piaaaaah... awamu hii na timu yetu tatakuletea salad ya ukweli pale pale uwanjani.. hii sio ya kukosaaaaa.

Tuesday, June 19

Nyama choma na Mtindi.

Sio kila mara wapaswa kula lunch ya menu kuuuuuubwa... muda mwingine unaweza kuagiza mtindi,  nyama choma kidogo na kachumbali.. na siku yako ikaisha kwa Amani.

Monday, June 18

Wali Dagaa.

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam huwa wanakula vyakula vya aina mbalimbali, basi MT ikawapata wapishi wa wali dagaa, wakatupatia mlo wa mchana.
 Hapo pana dagaa, mchicha kidogo na maharage... ebu jaribu kula hii leo.

Sunday, June 17

Vitafunwa.

Tunapohudhuria vikao mbalimbali, viwe vya harusi ama shughuli za kikazi, huwa kuna muda wa kujiburudisha ama kwa mlo ama kinywaji. Basi MT katika moja ya shughuli ya kikao ikapata wasaa wa kuona menu, kama kawa bila ajizi na sisi tukaamua kukushirikisha yalojili japo kwa picha tu.
 Hapo MT tulipata kuonja Menu ya viazi vya kukaanga na nyama ya kukaanga. Unataka nini Duniani zaidi ya Menu. Karibu Tena Hapa.

Friday, June 15

Jiko.

Katika mapishi ya kila siku huwa tunatumia saaana majiko, yapo majiko ya aina mbalimbali na hutumika kupika vitu na vyakula vya aina mbali mbali kutegemea na matakwa ya mpishi. katika tembea tembea yetu kitaa mara huku mara kule tumegundua kuwa wapishi wa chips mayai hawana design nyingine ya jiko la kupikia kiepe yai a.k.a zege ila hii.
Wewe je watumia jiko gani kuandaa menu yako? tujulishe menutimes@gmail.com

Sunday, June 10

Zege

Kunazo njia nyingi za kuandaa kiepe yai a.k.a zege, zege mara nyingi huwa na idadi ya mayai mawili, basi jamaa wa Calabash Pub Pale Mwenge Mpakani aliiandaa Zege moja matata sana na akalilemba kwa saladi taamu.... na sisi watu wa menu tukamtime.
 Ebu mfanyie timing mkaanga zege hapo jirani ujilambe kimenutime. Jifunze kula kwa muda.... Time The Menu..

Mchemsho wa Ng'ombe.


Katika pitapita za watu wanaojua kutime menu wakapita sehemu yaitwa Calabash Pub, Iko mitaa ya Mwenge Mpakani, Tukapata kuonja mchemsho wa ndizi pale, ah kiukweli ni mtamu, MT itaendelea kukuletea Menu za kila pahala, usikose kutumbelea badae kidogo.

Friday, June 8

Ugali nyama na mbogamboga.

Wale wanaojiita mabachela wajua ni wagumu sana kupika, lakini ishukuliwe MT baada ya kumshawishi Kaka Steve, ambaye ni Bachela timu ya MT ilimtembelea na kumuomba atuandalie msosi wa usiku...Basi bachela Steve akaamua kutupikia Ugali na Nyama ikisindikizwa na mbogamboga pamoja na Tunda (ndizi)






 Saa zingine unaziacha picha ziongee.. karibu Menu Time.. ukipika tupigie simu tuje kupata picha yako pia... 0715443434

Wednesday, June 6

Chips Mishikaki.

Marafiq wa MT wanazidi kututumia picha mbali mbali za Menu walizokula ama zilizowavutia, Leo tumepata Picha kutoka kwa Mdau mpya wa MT, Mr. Ramadhani a.k.a Baba Salha kutoka Mikocheni, Hiki ndicho alichopenda wadau wengine wa MT waone pia.
Usisite kututumia picha yako pia, leo chukua kamera yako, piga picha mlo wako, kisha tutumie menutimes@gmail.com.

Mchemsho toka Songea

   Raha ya kusafiri kwa timu ya Menu Time ni kupata wasaa wa kujaribisha menyu mbalimbali toka mikoa mbalimbali. Toka Songea kwenye Hotel yajulikana kwa jina Heritage Cottage, tulikutana na mchensho huu wa ng'ombe.

Hapa ndo upo chomboni tayari kwa kupakuliwa ili uweze kuliwa na walaji toka timu ya MenuTime na marafiq wa Songea

Kwa karibu zaidi ili nawe uweze kufaidi kuona vipande vya nyama vilivyopendeza

Hapa ikiwa tayari imepakuliwa katika bakuli la mmoja wa wanatimu wa Menu Time tayari kwa kuliwa.

  Waweza kula mchemsho huu ukichanganya na chapati au andazi yaani wewe tu na mapenzi yako.

Kutoka Songea mjini, LJM wa Menu time naarifu

Tuesday, June 5

Wali, maharagwe na mchuzi wa Nyama.

Marafiki wa Menu Time wanaendelea kututumia Picha mbalimbali, na leo tumepata picha kutoka kinondoni.
Rafiq ametutumia menyu yake ambayo ni wali wa nazi, maharagwe ya nazi pamoja na mchuzi wa nyama.


 Picha hii imetumwa na Rafiq yetu Muzakiru Ismail. MT inakushukuru sana kwa kushare nasi picha ya mlo wako.

Monday, June 4

Mchemsho wa Ndizi.

Menu yaitwa Mchemsho wa ndizi, picha hii imeletwa Menu Time na Rafiq aitwae Prolimina. 

 

Asante sana Rafiq Prolimina kwa kushare nasi picha yako.
Iwapo nawe ungependa kushare nasi picha zako, tafadhali zitumia kupitia menutimes@gmail.com nasi tutaziweka hapa zionekane na marafiq wa Menu Time popote walipo.

Sunday, June 3

Kiepe Mbuzi Choma.

 Hizi ni Menu za hapa na pale katika jiji la Dar es Salaam, wajua watu wengi hawapati muda wa kupika chakula chao wenyewe, hivo huwalazimu kupita katika migahawa ya vyakula na haya ni baadhi tu ya mambo yanayopatikana Dar es salaam.
  Tumekutana na sahani yenye chipsi, nyama ya mbuzi iliyochomwa, kachumbari kidogo ya kushushia mlo, na pilipili kwa waleeee wapenzi wa pilipli. Ndimu na chumvi vyasindikiza mpango mzima.....tunaamini Rafiq aliyekua anakula menyu hii alifaidi sana.

 Hizi ndo njia zetu jamani, popote tunapopita tunachukua matukio na kushare na marafiq zetu. Hii ndio MT, Karibuni Menu Time.

Ndizi na Mbuzi Choma.

  Ukiwa unaenda Tabata Segerea, kuna Kituo chaitwa Baracuda, na pale Baracuda kuna Bar moja maarufu sana yaitwa Baracuda Bar, basi katika pita pita zetu Timu ya Menu Time ikajikuta tu imefika mitaa ya hiyo na kujipatia mlo wa Ndizi mzuzu na nyama ya Mbuzi ya Kuchoma.
  Kama kawaida visindikizio kama kachumbari, pilipili, ndimu na chumvi haviwezi kukosekanika


 Baracuda Bar kwa kweli wanajitahidi kwa kiwango kikubwa tu. Tenga muda wako ukajipatie aina mbalimbali za chakula. Tufuate Menutime katika www.twitter.com/menutimetz na www.facebook.com/MenuTime

Samaki Sato

  Aina hii ya samaki hupatikana ziwa Viktoria pekee, ni samaki watamu ukiwala katika mapishi ya aina zote, tunaongelea wa kukaangwa, wa kuchemshwa, na hata wa kuungwa na mchuzi pia. Hapa Timu ya Menu Time imeletewa zawadi kutoka Mwanza, na Kama ilivo ada Timu yetu imeamua kukuonesha namna mbalimbali za kumpika ama kumtayarisha samaki huyu.

Uzuri aliletwa tayari ashakaangwa, kama aonekanavyo hapo chini

 Sasa waweza kumuandaa kwa kumpasha moto, kisha katakat kachumbari yako na kumla samaki huyu kwa kachumbari.

 Pia waweza kumuandaa ukamla chukuchuku, mchukue samaki wako, muoshe, kisha muweke kwenye sufuria weka na maji kidogo na pili pili, mchemshe mpaka maji yawe rangi ya njano hivi.
  Baada ya hapo pakua kwenye sahani au Bakuli tayari kwa kula.
 Ni samaki mtamu sana, pia wakati wapata kula samaki wako, waweza kujisindikizia na ugali, wali, chapati, yaani ni wewe tu na kile upendacho. Ukija kwenye kishushio ama tuseme kimiminika, waweza tumia juisi, chai, maji, soda na kdhalika..... je wewe wapenda nini? Tafuta samaki wa Sato kisha jaribu aina hizo za upishi tulizokuwekea hapo juu, kisha tutumie picha ya mlo wako ulifananaje kupitia menutimes@gmail.com . Karibu Menu Time.

Friday, June 1

Senene

 Hawa ni viumbe maarufu  sana huko Mkoani Kagera na wanaheshimiwa sana, ni mlo wenye historia nzuri ya kimapenzi tuseme. Ni hivi ukiona mchumba wa kihaya kakuletea hawa viumbe kwenye kisosi basi ujue siku ya kurudisha hicho kisosi, shurti kuwepo na kitu au vitu vya gharama sana. Picha hii imetumwa na kaka yetu pia Rafiq yetu wa kutoka mikoa hiyo, ila kwa sasa anaishi Kigoma.

 Asante Victor mashobe a.k.a Baba Ruge"Ronny".
Endelea kututembelea, na kututumia picha za menu kadhaa kutoka Kagera hadi Kigoma. Karibu tena tena na tena.