Sunday, October 28

Menyu za Shieni bar - Vuruga

   Moja ya siku zilizopita, nilikua pale Shieni na marafiq kadhaa, wengi wakiwa wamekuja kuonja mapishi ya Menu Time katika eneo hilo.
   Da Sia alitoa oda ya supu ya ng'ombe na akapatiwa. Supu hiyo ina viungo kadhaa vikiwemo njegere, viazi, nyama yenyewe, karoti nakadhalika.
   Picha ndo hii hapa, ofcourse chapati ni pale ambapo unapohitaji pembeni ya supu, ukiondoa chapati, waweza ulizia ndizi chemsha, choma n.k

   Epphy yeye aliagiza maini na firigisi vuruga. Hii yaitwa hivyo hivyo Shieni maini+ firigisi vuruga. Ila waweza ulizia maini vuruga peke yake, firigisi vuruga peke yake, au mchanganyiko wa maini na firigisi pamoja kama alivyofanya Epphy. Baada ya mapishi hayo, huchanganywa na viazi vilivyokaangwa a.k.a chips na kuandaliwa kama inavoonekana
 
  Tukujuze uchakavu kabisaaaaaa, ili ukielekea pande zile uwe umejipanga vyema.
Supu  ya ng'ombe ni sh 3,000/- tu, maini vuruga ni 3,000/=, firigisi vuruga ni 4,000/ za kitanzania.
   Karibuni sana shieni bar iliyopo Sinza mori.... upate moja ya milo hiyo hapo juu na mingine mingi ambayo tutaendelea kuwajuza taratibu.
   Kutoka Menu Time, tunawatakia wiki njema yenye mafanikio zaidi.

No comments:

Post a Comment