Saturday, October 27

Mbuzi na Ng'ombe za Kinondoni

   Menu Time tuna marafiq kila kona ya Dar es salaam, Tanzania, ndani ya Africa mpaka nje ya Africa. Tukirejea hapa nyumbani, tunapita pande za Kinondoni ambapo huku pia kuna marafiq ambao huwa tunakutana nao mara kwa mara katika shughuli za biashara ya vyakula.
   Sasa ukifika pale Kinondoni, nyuma ya Best bite, (naamini tulishawahi kupaongelea siku za nyuma) utakutana na hawa wapishi mashuhuri wa nyama ya mbuzi pamoja na ng'ombe.
   Uzuri wa nyama hii ni kwamba yapikwa katika utaalamu wa pekee ambapo unapokuja kuila waikuta ni laini mnoo, yaani yateleza mdomoni
   Nakuonesha ushuhuda wa nyama nayoiongelea, halafu nakujuza wapi eneo lilipo.
Tunaanza na nyama ya ng'ombe.....
 
Na hii ni ya mbuzi, si unaona mbavu zilivyopendeza
 
    Maelekezo yanaanzia pale best bite...... sasa basi fika best bite, kata ile kona kama waenda Nyumbani lounge, achana na kona ya kwanza kulia, nenda mbele mpaka uikute kona ya pili. Kisha ifuate mbele kidogo utaona magari kadhaa na upande wa kulia ndipo ilipo hiyo bar. Sisi tunaiita bar hiyo mbuzini. Kihalali yaitwa "Kibo Business". Fika pale upatapo muda.
   Mmoja wa wana Menu time amewakilisha mada!!!

No comments:

Post a Comment