Thursday, October 25

Picha toka kwa Rafiq

   Bila kutujuza jina, eneo alilopo, siku wala historia nyuma ya picha hii, Rafiq alitutumia na kuamua kushare nasi. Menu Time team, bila ya ajizi tukafanya kama tulivyoagizwa na hilo ni kuonesha kila picha tunayotumiwa na marafiq zetu.

   Katika sahani ya Rafiq kuna ndizi zilizochomwa, kuna nyama iliyochomwa vyema kwa chini hapo, na pembeni kuna kachumbari yaonekana tamu muno, ikiwa na pilipili inayosindikizia msosi wote.
  Tunawatakia mapumziko mema ya weekend, na pia sherehe njema.

No comments:

Post a Comment