Tuesday, October 23

Vyakula vya majini a.k.a sea food

   Kutoka kwa Rafiq wa Menu Time aitwaye Dagobeth Sheyo, tumetumiwa picha hiyo hapo jana, ambapo amesema alikua anakatiza pande za feri akakutana na menyu hiyo. Kidhungu ingeitwa Sea food, maana hapo kuna kiumbe cha baharini tunamuongelea pweza na pembeni yake kuna pilipili ya kutosha kama kikorombwezo.

    Kama ilivyo ada, mpango uko hivi, unachukua kijiti hapo kwenye kikopo, unakamata kipande chako, unakichovya kwa pilipili kisha unakula. Kumbuka ukishaingiza mdomoni kipande cha pweza, ukamega hupaswi kurejesha kwenye pilipili tena,kwa sababu za kiafya zaidi. Ukimaliza kujisevia, kiuhalali unajihesabia unampatia muuzaji pesa yake, unasepa.
   Kutoka pande za feri, upepo unapovuma, Menu Time inamshukuru sana Dagobeth kwa kushare nasi picha hii.

No comments:

Post a Comment