Monday, October 22

Menyu za Shieni bar - Supu ya ng'ombe

  Moja ya vitu anapenda kufanya Lulu, mmoja wa wanachama wa Menu Time ni kupika. Na kila anapopika hupenda Rafiqs wajaribu upishi wake na kumpatia mrejesho nyuma, je, aboreshe vipi yaani apunguze au aongeze nini zaidi katika hiyo menyu atakayokuwa amepika.
   Sinza Mori kuna bar mmoja yaitwa Shieni, hii bar imedumu zaidi ya miaka kumi. Siku za mwisho wa wiki mwenzetu hupenda kwenda pale na kuonesha uwezo wake wa kupika. Tunafurahi katika kuonesha ujuzi wake, Shieni bar wamekubali mapishi yake ambayo tayari ameshawapatia na uzuri mapishi hayo yamepokelewa vyema na Rafiqs, wateja na wanafamilia wa Shieni bar pamoja na Menu Time kwa ujumla.
   Pishi la kwanza kabisa ni supu ya ng'ombe, najua utajiuliza je, ina nini cha mno.... si unajua siri ya mpishi. Karibu kuijaribu kwa kukuonjesha kidogo kwa picha kabla ya kujishauri uwatembelee lini.
   Pita asubuhi upate kama kifungua kinywa na chapati pembeni
 
  Na pia tukutane jioni wakati tunaweka mambo sawa tayari kwa kuanza yalee mambo ya mwisho wa wiki. Supu ina viungo vyote muhimu na cha mno nyama ya kutosha ambayo ni fresh kabisa.

  Tukutane Shieni bar kila siku na haswaaaaa mwishoni mwa wiki upate kujaribishe menyu tofauti tofauti toka kwa mwana Menu Time mwenzetu.
  Kutoka Sinza kwa wajanja, tunakutakia wiki njema!!!

No comments:

Post a Comment