Sunday, October 21

Karibu Ilala - Mandi ya mbuzi na Kuku

   Hakika Menu Time ina Rafiqs wengi ambao wanapenda kula vyakula mbalimbali, kiasi cha kutafuta menyu gani mpya, au tuseme ambayo haijazoeleka mtaani, kisha hutujuza sisi kwa nia na madhumuni ya kwamba tuende kuihakiki hiyo sehemu na kuijaribu hiyo menyu, kisha tuweze share na Rafiqs wengine kupitia hapa kwenye blog, katika facebook wall yetu tafuta Menu Time kisha jiunge nasi, pia kupitia twitter, tufuate menutimetz upate kujua matukio ya Menu Time pale yafanyikapo.
   Basi wiki iliyokwisha tulipelekwa pande za Ilala na George, tukiambiwa huko kuna menyu yaitwa Mandi. Ukiiangalia ipo kama pilau au biriani, lakini ni tofauti mno. Chimbuko lake ni kutoka Yemeni, na inaonekana kama hapo chini pichani. Karibu!!!
   Hiii ilikua mandi ya mbuzi, na hili ni sinia kubwa, kuna dogo la nusu yake pia wanapakua.

   Timu ilikuwa na Rafiqs wengi, hivyo baadhi tulichagua kupata ladha ya mandi ya kuku. Anapikwa kuku mzima kama wachukua sinia kubwa, na nusu kwa sinia dogo. Unaona mambo hayo????
 
  Sasa huu mlo hauna mafuta kiviile, na walaaaa si mkavu pia, ila unapoagiza, basi ile supu iliyopikiwa hutengwa, kisha kuwekwa kwenye vibakuli na kuletewa pembeni kama ionekanavyo kwenye picha. Hiyo nyekundu ni pilipili..... tunatafuta imetengenezwaje maana laaaah, ziliagizwa bakuli si chini ya sita za pilipili na zote zilikwisha. 
 
   Nilichopenda kuhusu hii menyu, kwanza yaliwa na mkono, hakuna vijiko wala uma, ushatusoma? Kisha unachagua wataka kukaa kitako jamvini au kwenye kiti. Sisi tulichagua kukaa kitako, maana wanasema ukienda Italy ishi kama waitaliano. Tukaketi jamvini tayari kwa kula hiyo mandi ya kuku na mbuzi.
 
  Kwa ukaribu kabisa hii ndo pilipili iliyozingua timu nzima, maana inautamu na papo hapo inawasha kwa mbali. Ni tamu mno kuila na mandi, na naamini hata kwa chakula kingine kile, kama sio peke yake.

Hii menyu yapatikana Ilala, narejea tena kusema sio biriani wala pilau ni mandi. Ni menyu ambayo yapasa kuijaribu. Tumeonesha ramani unafikaje huko walipo katika facebook wall yetu .
  Nenda kaijaribu kisha rejea tujuze wewe umeionaje. anwani zetu ni zilezile info@menutimetz.com au menutimes@menutimetz.com
   Menu Time yasema George asante sana kwa kutufikisha mandi restaurant, na kutoka Ilala twasema Jumapili njema

No comments:

Post a Comment