Thursday, October 18

Makange ya Kuku!!

   Jana nikiwa na mmoja wa Rafiqs wetu wa Menu Time aitwa Fatma a.k.a Fettiyish tuliamua kukutana pande za Rose garden a.k.a RG kuongea moja, mbili, tatu.
   Yeye akiwa na hamu ya kula mbuzi, nami nina hamu ya kula makange ya kuku. Tukafika, tukaagiza..... tusiseme sana, ila tulicholetewa ndicho haswa tulichotegemea, na ndo hicho mnachokiangalia......
   Sahani yangu iliwa na makange ya kuku nusu na mbogamboga zake!!!!
 
      Sahani ya Fettyish ikiwa na mbuzi, pande liitwalo jembe,

 Ukiondoa nyama pia tuliagiza ndizi mzuzu za kuchoma na kasalad ka kushushia menu hiyo. Vunywaji was maji baridi, soda na Redbull.
     RG panajulikana na uwepo wa menyu ya maana, na kutoka Menu Time team tumehakikisha na kukubali hilo, hivyo pass by pale, upate kokoto, makange, chipsi, samaki na mengineyo mengi. Wapo Sayansi Rose garden Rd.

No comments:

Post a Comment