Wednesday, October 17

Mlo wa Usiku toka pande za Oysterbay

   Moja ya maeneo huwa naenda kwasababu ya chakula chao ni Q-bar. Hawa Rafiqs, jiko lao liko makini zaidi ya unavyodhania. Ukiondoa umakini wa jiko, pia wahudumu hutoa service nzuri ambayo itakuacha na certain satisfaction, ngumu kuielezea...... cha mno, itakupa hamu ya kurudi tena kupata mlo mwingine.
    Wapo mitaa ya Oysterbay na ukiondoa vyakula, kuna vinywaji pia ni bar maarufu sana sana kwa kuonesha michezo mbalimbali kupitia luninga zao zilizowekwa kila kona ya eneo hilo.
    Rafiq kutoka UK (sio Ukonga) alifika Dar na katika pitapita zetu akatamani chakula kitamu, na kutokana na kwamba tulikua pande hizo, takaingia na kupata mlo wa usiku.
   
Yaliyojiri ndo haya:
 Hii ni sahani yake ambapo kuna wali mweupe, chipsi kiasi, salad ya kusindikizia na nyama iliyowekwa sosi yake kwa juu tayari kwa kuliwa.
 
   Sahani yangu ilikua na viazi vya kuponda a.k.a mashed potatoes, nyama ya nguruwe iliyookwa vyema na salad ya kusindikiza mpango mzima.

   Pamoja tulishushia na mvinyo mwekundu a.k.a red wine. Kisha kilichofuata  tukawashukuru wahudumu kwa ukarimu wao, of course tulilipa, tukasepa. Kama una mgeni au pasi mgeni umejisikia kupata chakula kitamu na upo pande za Oysterbay, pita hapo Q-bar halafu agiza chakula chochote tu, tunakuguarantee utapata utamu wa kutosha.
Tips: Jaribu mishkaki yao pia....... halafu njoo turejee tujuze!!

No comments:

Post a Comment