Monday, October 15

Mambo ya Weekend

   Napokua na marafiq siku za mwisho wa wiki a.k.a weekend, huwa tunachagua je, tukajaribu menyu ya upande upi?. Na maamuzi haya hutolewa na mmoja wetu na kuafikiwa na wengine.
   Jumamosi iliyopita tukajikuta katika moja ya sehemu inayofahamika sana hapa Dar na pengine ufahamikaji wake unachangiwa na jina la sehemu yenyewe.
   Panaitwa "Simba kapakatwa bar", hawa wapo mitaa ya Makumbusho na wana eneo zuri , lenye hewa safi na sehemu kubwa tu ya kupaki usafiri wako. Kilichotupeleka pale ni menyu yao, ambapo tulikutana na hii hapa...

 
  Ni nyama ijulikanayo kama kitimoto, ikiwa na ndizi zilizokaangwa, pembeni kuna pilipili ya kusindikizia. Hii imechomwa na ikachomeka vyema. Niliipenda na naamini ntarejea na Rafiqs wengine pale.
   Ukiwa mitaa ya Makumbusho, Dar es salaam, fanya kupita hapo.
Shukrani sana kwa familia ya Victor Mashobe kwa kunipeleka pale pamoja na Robert. Tujuze je, weekend yako ulikula nini na wapi?.  info@menutimetz.com ndo anwani yetu.

No comments:

Post a Comment