Katika harusi mbalimbali na sherehe mbalimbali, hakuna sehemu muhimu
na inayopendwa na watu wengi kama muda wa msosi a.k.a Menu Time, Uncle
Ringo na Aunt Anitha Jumamosi ya tarehe 23 June 2012, walizikonga nyoyo
zao kwa kufunga pingu za maisha, zilizofuatiwa na sherehe kubwa na ya
kistaarabu iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, MT ilishuhudia
mwanzo mwisho idara ya maakuli na hii hapa ni exclusive coverage ya
Mnuso wa Uncle Ringo.
Ndafu
ni moja kati ya menu nyingi zilizokuwepo, Mshereheshaji wa siku hiyo
alitoa historia ya kitu hii kuitwa ndafu na kusema kuwa, hii ilitokea
baada ya Mzungu mmoja kukaribishwa Menu Hii huko Moshi, Baada ya kuiona
tu na kuionja mzungu wacha maneno yamtoke, akasema "This is Wonderful" wakazi wa Moshi waliokuwepo eneo
hilo wakasema Mzungu kaiita "Ndafu", Kuanzia siku hiyo mpaka leo Hii
kitu inaitwa Ndafu.
Hatukuishia kwenye ndafu tu, tulienda hatua nyingi mbele zaidi tukakutana na kitu cha Buffet, wali mweupe a.k.a majimaji ilikuwa nambari wani.
Bila wali mchafu a.k.a Pilau sidhani kama viwanja vya Karimjee vingekalika ha ha ha ha sherehe bila pilau haijatimia.
Wale wenzangu na mimi wa ndizi hawakusalimika kwenye Buffet la Mnuso wa Uncle Ringo, Acha watu wajilie kitu cha ndizi.
Kabla sijaelewa nini kinaendelea mbele yangu nikakutana na vipande vingi vingi vya kuku, acha niduwaee, ama kweli macho yatashindwa kutambua vitu vingine lakini sio chakula.
Ng'ombe nao hawakusalimika, ilibidi wachinjwe na wapikwe Rost, ali mradi Kusherehesha Harusi ya Mr& Mrs. Ringo.
Wataalamu wa chakula wanayaita Macaron, matamu hayo.
Ki ukweli aina nyingi za vyakula zilikuwepo na ulikuwa huru kuchagua mlo uupendao, Samaki walokatwa vipande vipande, wakakaangwa, kisha wakaandaliwa na mchuzi, niliionja na ilikuwa tamu mno.
Mboga mboga na Kisamvu pia vilijumuishwa kwenye Mnuso.
Salad iliandaliwa ya kutosha na mtu alikuwa huru kula salad aipendayo, chagua ya kwako na wewe kati ya hizi.
Dah! mimi niliridhika na maandalizi ya sherehe nzima na lilipokuja swala la Menu niliwakubali sana waandaaji. tupe mtazamo wako na wewe. Kama una sherehe yako na ungependa Menu Time tuiripoti wasiliana nasi.
No comments:
Post a Comment