Tuesday, December 17

Menu ya Sinza

Jana jioni tuliona ni vyema kwenda salimia Rafiqs waliopo pande za Sinza, mkabala na Lion's hotel, ulizia kwa Tobby lakini maarufu kwa jina lake ambalo ni Spotlight pub.
  Eneo ni tulivu na baada ya kuketi tulivutiwa na harufu taamu ya menu iliyokuwa yatokea pande za jikoni. Team ya Menu time tukahoji je ni nini chapikwa?? tukajuzwa ni mchemsho wa ng'ombe na hapo chini ndo ushahidi wa picha


  Sasa wakati tunauliza vya juu yaani mchemsho wa ng'ombe, tukapishana na sura ya nyama ya mbuzi juu ya jiko, mate yakamwagika, moyo ukatamani na meno yakajitayarisha, na chini ndio nyama tuliyoagiza.

   Sehemu iko vyema, menu zake zipo sawa, ni pahali pa kwenda iwapo una hamu ya mchemsho wa ukweli wa ng'ombe au hata mbuzi iliyochomwa ikachomeka vyema.
   Disemba ndio hii, mwezi wa nyama nyama nyaaama.

No comments:

Post a Comment