Wednesday, September 26

Mboga mboga time

   Kwenye kila mlo, ni vyema kuweka mbogamboga za majani, ili kukamilisha lishe bora. Kuna aina nyingi za mboga za majani, mathalani spinach, mchicha, matembele na kadhalika, ambapo inategemea na nini umeandaa kutokana na mapenzi yako.
  
 
   Katika mlo wa leo, kuna spinach,  bamia zilizochanganywa na nyanya chungu na kuungwa pamoja kisha kuna kachumbari ambayo ina mchanganyiko wa vitunguu maji, nyanya, pilipili hoho, chumvi kwa mbali na ndimu.
   Mboga hizi huweza kuliwa na mlo wowote iwe ugali, wali, viazi au yenyewe yaani ni wewe tu mapenzi yako.
   Kama una namna ya kupika aina ya mboga tujuze kupitia info@menutimetz.com au menutime@menutimetz.com nasi tutawajuza wengine. 

No comments:

Post a Comment