Wednesday, April 9

Arachuga by Night

  Ilipotimu mida ya usiku, wenyeji wetu wakatupeleka sehemu mbalimbali ili kuiona Arusha mida ya usiku ikoje? Moja ya sehemu tulikwenda ni Club D ambapo ni pazuri, pana ukumbi mkubwa, nafasi na hewa, Rafiqs wanacheza kwa nafasi na pia huduma ni nzuri.
  Ila kabla ya kufika hapo Club D, tulipata wasaa wa kupita Babylon ambapo kulikua na Rafiqs wengi, muziku mzuri lakini haswa menu tofauti.
  Hapa tulipata kuonja utumbo uliokaangwa na viungo mbalimblai na hakika ulikua mtamu mno. Hii kuna haja ya kuijaribu nyumbani itakuaje
                               
  Tulisindikizia menu hiyo na ndizi tamu, huku vimiminika kadha wa kadha vikisindikiza. Naamini kiungo kimoja maalumu na muhimu katika menu hii ni pilipili, maana kwa mbali ilikua inawasha lakini kwa utamu.
   Asante zetu ziwafikie Victor Mashobe, Kii pamoja na Tumaini a.k.a Tumaa kwa kutujali, kutuangalia na kutuonjesha menu tamu za Arusha.
   Tukaaga wana Arusha, tukaelekea Moshi ambapo tutakujuza zaidi kesho.

No comments:

Post a Comment