Thursday, April 10

Kifungua kinywa - Meku's Bistro

Baada ya kupata cha asubuhi na mchana kutoka pande za Arusha, na kuiona vyema Arachuga by night, Alfajiri tukaamkia Moshi ambapo tuliwafuata wenzetu, na ukaribisho wa Moshi ambapo ndio home pia, ulikua kama ifuatavyo:
  Kulikua na supu ya mbuzi, ya moto na tamu kwelikweli yenye viungo kadhaa pia, na ushuhuda ndio huu

Pia kulikua na mtori, na kilichonifurahisha zaidi ni wingi wa finyango za nyama. 
Ila kama vile nyama hazikupikwa na mtori, huwa silielewahi hili, kwa maana nyama iliyopikwa ndani ya mtori inapata ladha flani ya kiutofauti hivi na tamu zaidi.
                  
  Baada ya kufungua kinywa, tukapumzika kidogo, kisha tukapandisha Rombo mkuu kwa bibi, pamoja na Kilalaracha kwa Rafiqs. Tutakuja wajuza walojiri

No comments:

Post a Comment